NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

KAMATI ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bagamoyo ,,imeiasa halmashauri ya Chalinze kuongeza usimamizi na jitihada ili kuinua ukusanyaji wa mapato yake ya ndani.

Kwa miaka miwili mfululizo halmashauri hiyo imesifika kwa ukusanyaji mzuri unaovuka malengo lakini kwa taarifa kutoka wizara ya TAMISEMI inaonyesha haimo kwenye halmashauri bora kwa ukusanyaji wa mapato .

Mwenyekiti wa CCM Bagamoyo,alhaj AbdulZahoro Sharif alisema ,kamati hiyo imelazimika ,kukutana na wakuu wa idara,wataalamu na madiwani wa halmashauri hiyo,kuangalia endapo kuna mapungufu ama mianya yaliyosababisha kushuka kwa makusanyo hayo ili yadhibitiwe .

Alisema kamati haijaridhishwa kwa kushuka kwa ukusanyaji wa mapato ya halmashauri ya Chalinze, kipindi cha mwaka 2017/2018 hivyo ijitahidi kusimamia vyanzo vyake vya mapato."Achane kufanya kazi kimazoea ,usimamizi sio mzuri ,;" bado sijaridhishwa na hali ya makusanyo na mtasababisha ilani kushindwa kutekelezeka kwa wakati ,alisema alhaj Sharif.Aliwataka washirikiane baina ya wataalamu, watendaji na madiwani kwa pamoja kubuni vyanzo vipya vya mapato.Kwa upande wake ,mweka hazina wa halmashauri ya Chalinze (DT) David Rubibira alisema kwa siku moja wanakusanya makusanyo katika malori ya kokoto 197-200 ambapo kwa siku wanakusanya sh.mil.8.9 .#

Ofisa mipango wa halmashauri ya Chalinze ,Shabani Millao alisema ,kuhusu suala la kushuka kwenye makusanyo ya mapato ya halmashauri hiyo linatafsirika sivyo kwani wapo vizuri katika makusanyo .Millao alitaja sababu za kutofikia kwenye makusanyo kwa kipindi hiki kuwa ni pamoja na kushushwa kwa makusanyo ya mazao ya chakula yasiyozidi tani moja ,na kuzuiwa kwa ushuru wa mabango .Alisema ,wamejipanga kurekebisha makadirio hivyo watafanya maotei kutegemeana na hali halisi ya makusanyo kulingana na chanzo husika.

Kwa upande wake ,mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Saidi Zikatimu alifafanua ,ukusanyaji 2016/2017 walikusanya kiasi cha sh .bilioni 3.800 wastani wa asilimia 118."Tukaona kama tumevuka lengo tukaona tujiwekee malengo ya juu na tuongeza ongezeko la asilimia 26 ambalo tumekisanya sh.bilioni 4 badala ya kukusanya bilioni 4.3"alisema Zikatimu.

Alisema, katika malengo ya mwaka huo manake walivuka lengo kwa kukusanya kwa asilimia 17 badala ya asilimia 26 .Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ,Amina Kiwanuka alisema wamepokea maagizo yaliyotolewa na kamati hiyo na wataifanyia kazi ili kuboresha makusanyo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Saidi Zikatimu,akitoa ufafanuzi wa jambo wakati kamati ya siasa ya CCM Bagamoyo ilipokwenda kukutana ,kuzungumza na wakuu wa idara ,wataalamu na madiwani wa halmashauri ya Chalinze .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Wajumbe wa Mkutano
Mwenyekiti wa CCM wilayani Bagamoyo ,alhaj Abdul Sharif akizungumza na wakuu wa idara ,wataalamu na madiwani wa halmashauri ya Chalinze (hawapo pichani),wa kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Saidi Zikatimu.(picha na Mwamvua Mwinyi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...