Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

Mkurugenzi wa Masoko Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Ernest Mwamwaja amesema kuwa maonesho ya Swahili International Tourism Expo SITE yameweza kukutanisha wadau wa utalii. 

Maonesho hayo yamewakutanisha wafanyabiashara katika sekta ya utalii waTanzania, nchi za Afrika Mashariki na wakala wakubwa kutoka nchi tofauti duniani. 

“Tumepata mawakala wa Utalii kutoka sehemu mbalimbali duniani na wameweza kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na wafanyabiashara wa sekta ya Utalii na kuwapa fursa ya kutangaza bidhaa zao,”amesema Mwamwaja. 

Mwamwaja amesema kuwa maonesho haya yameweza kuleta fursa kwa wafanyabiashara wa sekta ya utalii wa hapa nchini na mawakala hao ambao ndio wadau wakubwa wa utalii duniani. 

Amesema kuwa, kwenye maonesho haya yameweza kuchagiza zaidi kwenye sekta ya utalii ambapo kwa mwaka huu kumekuwa na vivutio vipya zaidi hasa kutoka Kusini mwa Tanzania hususani kwenye Mkoa wa Iringa kukiwa na mazao tofauti ya utalii. 

Mwamwaja amesema kuwa, wameamua kuja na kauli mbiu ya Tanzania Unforgetable wakiwa na malengo ya kuendeleza mazao ya asili yanayopatikana kusini mwa Tanzania, na kwa sasa wameweza kufanya mazungumzo na benki ya Dunia na kuwapatia mkopo wa Dola za kimarekani 150 kwa ajili ya kuendeleza mazao ya utalii kwa vikundi vidogo vidogo . 

“fedha hizo zimeweza kuwezesha kuwapa fursa vikundi vidogo vidogo kutoka ukanda wa kusini na utaona kuna upande mzima kuna mabanda yanayoelezea mazao ya utalii yaliyopo kwa kusini wa Tanzania,” 

Kwa mwaka huu, TTB wamewezesha makundi maalum ya wakina mama na walemavu kushiriki moja kwa moja katika maonesho hayo, wameweza kutumia wabunifu wa Tanzania kwa ajili kubuni mavazi waliyovaa na zawadi kwa washiriki wa maonesho hayo. 

“Tupo katika kuandaa studio itakayokuwa inaandaa vipindi tofauti vya utalii na hili litasaidia kukuza sekta ya utalii, ukiachilia hilo tuna mitandao ya kijamii ambauo inaweka taarifa mbalimbali za TTB na utalii kwa ujumla”amesema Mwamwaja. 

TTB wameamua kuwapa fursa washiriki wa maonesho hayo safari za kutembelea sehemu mbalimbali na kuwaonesha mtawanyiko mpana wa utalii wa nchini kwetu na kuweza kufahamu Tanzania ina vivutio vingi zaidi na pindi watakaporejea nchini kwao wakatangaze. 

Baadhi ya maeneo watakayotembelea ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Ruaha, Mikumi, Udzungwa, na Tarangire, bonde la Ngorongoro, visiwa vya Zanzibar na Mafia pamoja na fukwe ya Pangani.Aidha onesho hili pia hutumika kama fursa ya kutangaza Utalii wa ndani ambapo watoa huduma za Utalii wa Tanzania huweza kuhamasisha wageni wanaotembelea onesho la S!TE kutumia huduma zao na kutalii sehemu mbalimbali nchini pamoja na kujifunza fursa mbalimbali za sekta ya utalii. 



Wadau mbalimbali wa utalii wakiwa wamefika kupata taarifa kwenye mabanda ya maonesho ya kimataifa ya Utalii Nchini wahili International Tourism Expo (SITE) yaliyoanza Okotba 12 hadi 14 yakiwa yameweza kukutanisha washiriki 300 kutoka sehemu tofauti duniani.
Banda la Vizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakiwa washiriki wa maomesho ya kimataifa ya 






















Utalii Nchini wahili International Tourism Expo (SITE) yaliyoanza Okotba 12 hadi 14 yakiwa yameweza kukutanisha washiriki 300 





















kutoka sehemu tofauti duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...