Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amezindua mradi wa uchakataji majitaka wa Toangoma Wilaya ya Temeke.

Mradi huo uliotekelezwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) na Shirika la PDF chini ya Shirika la Water Aid Tanzania.

Akiwa katika mradi huo, Aweso amezindua mradi huo ukiwa na vipengele vikuu vinne ambavyo ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma za uhifadhi na udhibiti wa taka ngumu kwa wakazi wa kata 23 za Manispaa ya Temeke.

Mradi wa Tuangoma umetumia kiasi cha Milioni 359 ukijumuisha ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali ambayo ni pamoja na  sehemu ya Kuchujia taka ngumu (screening chamber), tenki la kuhifadhia majitaka kwa muda mrefu (balancing Tank), mtungi wa kuchakata majitaka na kutengeneza gesi (biogas Dome) sehemu ya kuchujia majitaka (perforated grave  filter) na sehemu ya kukaushia tope la majitaka.

Mtambo huo una uwezo wa kuhifadhi majitaka kiasi cha lita elfu hamsini (50m3) na uwezo wa kuhudumia wananchi 93,000 na uwezo wa kuzalisha gesi kiasi cha lita 4000 kwa siku ambayo inaweza kuhudumia takribani kaya 250 kwa mwezi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani hususani kupikia.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi wa mradi wa uchakataji majitaka Toangoma uliojengwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA)  na Shirika Shirika la PDF chini ya Shirika la Water Aid TanzaniaKushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mbagala Ally Mangungu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majitsafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja na Kulia ni Mkuu wa  Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva.
Mhandisi Elias Kazingoma kutoka Shirika la PDF (Kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso moja ya sehemu inayotumika kuhifadhia majitaka kwenye mradi wa Uchakataji majitaka wa Toangoma.
 Mhandisi Elias Kazingoma kutoka Shirika la PDF akimuelezea Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso mradi mzima wa kuchakata majitaka uliojengwa  Mamlaka ya Majisafi na Majitaka  (DAWASA) na Shirika la PDF chini ya Shirika la Maji la  Water Aid.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...