Ratiba ya Kumuaga mtoto  wa Mwalimu Mwakasege  aliyefariki Alhamisi October 11 :- Mwalimu atawasili Dar leo Jumatatu. Jumanne mwili utaagwa Mbezi Beach Lutheran Church, Jumatano alfajiri ni safari kuelekea Mbeya, na Alhamisi ni mazishi mjini Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
Mahali ulipo msibaL: - Msiba uko Dar kwa mdogo wake Mwalimu Mwakasege anaitwa Eng. Mwakasingila (Mzee wa kanisa wa KKKT Mbezi Beach)  Jinsi ya kufika msibani Fika hadi  Mbezi Beach Jogoo, unaingia barabara ya Karibu Art Gallery kuelekea TAG Mbezi beach kisha utaona vibao vinavyoelekeza msiba ulipo.  
Ratiba ya Jumatatu Kutakuwa na sara ya pamoja na Mwalimu Mwakasege na familia yeke yote itakayofanyikia hapa msibani itakayoanza saa moja jioni, 7pm itakayoongozwa na Askofu , Mchungaji kiongozi na watumishi wengine  Kuaga  Mwili wa marehemu utaagwa Jumanne 16 Oct kanisani KKKT Mbezi Beach Dar, kuanzia saa nane mchana (2pm)  Baada ya kuaga mwili utapelekwa airport kwa ajili ya maandalizi ya safari.  
Kusafirisha: Mwili utasafirishwa Jumatano 17 Oct kwa ndege  Mazishi:  Yatafanyika alhamisi, Tukuyu, Mbeya 18 Oktoba,2018.  
Muhtasari: Joshua amefariki ghafla baada ya  kudondoka  alhamisi tarehe 11 Oct 2018 akiwa kazini kwake World Bank Dar. Alikimbizwa Aga Khan hospital ila alifariki siku hiyo hiyo.
Mwalimu Mwakasege pichani kulia akiwa na Mtoto wake Joshua ambaye kwa sasa ni Marehemu.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...