Na Mwandishi Wetu Kibiti, Pwani
Wananchi wa Kijiji cha Mweyubaruti Kata ya Mwambao Wilaya Kibiti wametakiwa kujenga hali ya kujiletea maendeleo badala ya kusubiri serikali kwakuwa mwelekeo wa serikali ni kurejesha hali iliyopotea  ya wananchi kuchangia   maendeleo yao wenyewe. 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile amesema hayo wakati alipotembelea Kijiji hicho kujionea shughuli za wananchi kujiletea  maendeleo.

"Zamani wananchi walikuwa wanajenga shule wao wenyewe au kushiriki kwa kujitolea nguvu zao na serikali inataka kurejesha hali hii na huu ndio mwelekeo wa serikali". Alisema Dkt.Ndugulile.

Wananchi kwa kutumia nguvu juhudi zao wamefanikiwa ku 
anzisha  mradi wa  shule shikizi kwa ajili ya watoto wadogo ambao hawawezi kwenda umbali mrefu kuhudhuria masomo ya awali.

Wakati huhuo Katibu wa Kitongoji Kijiji hicho Bw. Alfan Matimbo akitoa taarifa Kwa Naibu Waziri Ndugulile  kuhusi  taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo alisema wanafunzi wamekuwa wakishindwa kuhudhulia masomo katika shule ya  Msingi Kivinje B kutokana umbali mrefu kwani shule hiyo iko umbali wa km.5 kutoka Kijijini hapo.

Aidha Mzee Matimbo aliongeza kuwa umbali wa Kijiji hicho na shule ya Msingi Kivinje B ni chanzo cha utoro kwa watoto wa Kijiji chake  lakini pia wanafunzi wengi wamekatiza masomo hivyo wananchi wamejipanga kujenga shule ili kuwezesha watoto wao kuendelea na masomo.

Aidha katika juhudi za kupambana na tatizo hilo Kijiji kinamlipa mwalimu wa kujitolea ambaye analipwa sh. 1500 kwa kaya kwa mwezi lakini pia wale wanaoshindwa kutoa fedha hii uchangia mazao ya chakula kama miogo na nanasi.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea Maelezo ya Mradi wa ujenzi ya Shule Shikizi iliyopo kata ya Mwambao Kijiji cha Mweyubaruti Kibiti Mkoani Pwani.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea mchango wa ujenzi wa shule ya Mradi wa ujenzi ya Shule shikizi iliyopo kata ya Mwambao Kijiji cha Mweyubaruti Kibiti Mkoani Pwani kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhiwa  mabati kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa shule shikizi iliyopo katika Kijiji cha Meyebaruti  kilichopo katika Kata ya Bungu Kibiti Mkoani Pwani. Picha Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...