Na Mwandishi Wetu,Globu ya jamii
SHILINGI bilioni tatu zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam ambapo ujenzi unatarajia kuanza Novemba mwaka huu.
Uamuzi wa kutengwa kwa fedha hizo ni katika jitihada za kuondoa changamoto zinazoikabili machinjio hayo.
Hayo ameelezwa jana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega.
Ulega alifanya ziara fupi katika machinjio hiyo akiambata na viongozi wengine wa serikali wakiwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Nyama, Dk wa Mifugo na Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko na uzalishaji toka Wizarani.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Ulega alielezwa changamoto zinazoikabili machinjio hiyo ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara wa nyama kutozwa ushuru mkubwa kwa mazao ya mifugo, ukosekanaji wa soko la uhakika la ngozi, ambapo Ulega amesema Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ina mkakati kabambe wa kukabiliana na changamoto hizo.
Ulega amefafanua kwa kuanza na ujenzi wa machinjio mpya ya kisasa utakaofanyika kwa gharama hizo za fedha za Serikali.
“Wasimamizi wote wa ujenzi wa machinjio hii nawataka muhakikishe kuwa ujenzi huu unafanyika kwa haraka na ubora ili machinjio hii iweze kuchinja ng’ombe, mbuzi, kondoo na kuku kwa kuwa machinjio nyingi zilizojengwa hazijazingatia suala la uchinjaji wa kuku,” amesisitiza Ulega.

Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega(katikati) akiwasili kwenye
eneo la machinjio ya Vingunguti kwa ajili ya kutatua kero mbalimbali
zinazowakabili wadau wa machinjio hayo jana jijini Dar es Salaam.(Picha
na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi
(wadau) wa machinjio ya Vingunguti kuhusu kero zao mbalimbali
wazipatazo kuhusu eneo hilo la Mchinjio.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na
wananchi(wadau) wa machinjio ya Vingunguti ambapo amewahakikishi
serikali ya awamu ya tano ipo pamoja nao na amewaomba kulipa kodi ili
kuinua uchumi wa Taifa.
Naibu
Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto
akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega
jana katika machinjio ya vingunguti jijini Dar es Salaam.
Wadau wa machinjio ya Vingunguti wakiendelea na kazi.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...