Na Mathew Kwembe.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amepokea magari mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200 na kusema kuwa magari hayo yataongeza thamani katika juhudi za serikali za kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Akiongea katika hafla ya makabidhiano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa USAID Tanzania David Thompson aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa dhamira yake ya kuboresha viwango vya afya kwa watanzania wote.
“Kupitia msaada huu, Serikali ya Marekani inaungana na Serikali ya Tanzania kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watu wote, katika jamii za watu wa Lindi na Mtwara, mkazo zaidi ukiwa kwa wanawake na vijana,” alisema.

Kabla ya kuyapokea magari hayo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) David Thompson, Waziri Jafo alisema kuwa anatambua kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Marekani kupitia Mradi wa USAID Boresha Afya kanda ya kusini.

Alisema kuwa kwa kutambua kazi nzuri inayofanywa na mradi wa Boresha Afya katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Njombe, Lindi, Mtwara na Ruvuma anayo furaha kubwa kushiriki katika hafla hiyo ya kupokea magari hayo yenye thamani ya Tsh.219, 372,136.

“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania ningependa kuwafikishia shukrani zetu za dhat kwa Serikali ya Marekani na wote walio katika mradi huu wa USAID Boresha Afya Kanda ya kusini,” alisema.Waziri Jafo aliongeza kuwa serikali inajivunia kushirikiana na washirika ambao kweli wanajali hali za raia wa Tanzania.Alisema kuwa kupitia msaada huo USAID Boresha Afya Kanda ya kusini imeonyesha kweli iko pamoja na watanzania katika kusimamia changamoto za afya nchini.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akizungumza wakati wa kupokea msaada wa magari mawili katika wizara hiyo yatakayotumika katika mikoa ya Lindi na Mtwara kupitia mradi wa USAIDS Boresha Afya Kanda ya Kusini.
 Kaimu Mkurugenzi mkazi wa USAID Tanzania David Thompson akizungumza kuhusu wanavosimamia miradi mbalimbali ya USAID hapa nchini Tanzania wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari mawili kwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Mkurugenzi wa Deloitte Consulting LTD, Carlton Jones akizungumza kuhusu wanavyosimamia mradi wa USAID Boresha Afya kanda ya Kusini unaotekelezwa katika halmashauri 43 kwenye mikoa ya Iringa, Njombe, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma wakati wa kutoa msaada wa magari mawili kwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
 Kaimu Mkurugenzi mkazi wa USAID Tanzania David Thompson (wa tatu kushoto) akimkabidhi mfano wa funguo wa gari Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo(katikati) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari mawili kwa Wizara hiyo leo Jijini Dar Es Salaam. Wa kwanza kulia ni Dk. Marina Njelekela, Wa Tatu kulia ni Mkurugenzi wa Deloitte Consulting LTD, Carlton Jones na wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI Dkt Zainabu Chaula.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...