Na Karama Kenyunko, glogu ya jamii

MAMLAKA ya hali ya Hewa nchini,( TMA) imesema mvua katika Mikoa ya Pwani ikiwemo Dar es Salaam zinatarajiwa kuanza Novemba 23 mwaka huu.

Pia TMA imetoa utabiri wa msimu wa mvua wa kuanzia mwezi Novemba 2018 hadi Aprili 2019 kwa mikoa inayopata mvua Mara moja kwa mwaka ambazo zinatarajiwa kuwa za juu na wastani.

Akizunguza wakati akitoa utabiri huo, jijini Dar es Salaam leo Oktoba 18, 2018, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Agnes Kijazi amesema mvua zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Kisini mwa mkoa wa Morogoro, Lindi na Mtwara. Huku maeneo ya mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Songea yakitarajiwa kuata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

"Kutokana na mifumo ya Hali ya hewa inayotarajiwa, mvua za wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka, maeneo yaliyosalia ya mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Songwe yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Amesema, mvua za msimu ni mahususi kwa maeneo ya magharibi mwa nchi, kanda ya kati, nyanda za juu kusini magharibi, kusini mwa nchi, ukanda wa pwani ya kusini pamoja na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro ambayo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.


Aidha Kijazi amezitaka sekta mbalimbali zinazotumia taarifa ya hali ya hewa katika kutekeleza majukumu yao kama vile, kilimo na usalama wa chakula, Afya, Mifugo na Wanyamapori, Maliasili na Utalii, uchukuzi na Mawasiliano, Nishati, Maji na nyingi za kuchukua taathari kufuatia mvua hizo nyingi kwani inaweza kusababisha madhara mengi katika Jamii nzima.


Kwani matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa yanaweza kupelekea maji kutuama na kusababisha mafuriko.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa taarifa za utabiri wa hali ya hewa ya msimu wa mvua leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utabiri, Samwel Mbuya na Mkurugenzi wa Utabiri TMA, Dk. Hamza Kaberwa (kulia).
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya Hewa nchini( TMA) Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mvua katika Mikoa ya Pwani ikiwemo Dar es Salaam zinatarajiwa kuanza Novemba 23 mwaka huu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya Hewa nchini( TMA) Agnes Kijazi  jijini Dar es Salaam leo kuhusu mvua katika Mikoa ya Pwani ikiwemo Dar es Salaam zinatarajiwa kuanza Novemba 23 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...