Na.Alex Sonna,Dodoma
Kufuatia ongezeko la magari
yanayoendeshwa na madereva wa Serikali kupata ajali, Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani Tanzania limeibuka na kutoa tamko la kufuatilia na
kuhakikisha madereva wanaoendesha magari ya viongozi wa Serikali
wanapata mafunzo ya kuwaendesha viongozi hao.
Akizungumzana na waandishi wa
habari Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Baraza hilo,Hamadi Masauni wakati akitoa tamko la
kwanza mara baada ya kuchaguliwa kwa baraza hilo huku akiwa ameongoza
na Makamu Mwenyekiti wa baraza,Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano,Elias Kwandikwa na wajumbe wengine wa Baraza hilo.
Mhe.Masauni amesema kuwa baraza
lilopita lilifanya kazi nzuri ila baraza jipya lina malengo yake ya
kupunguza ajali nchini hasa za viongozi wa Serikari kwa kuwafuatilia na
kuhakikisha madereva wanaoendesha magari hayo wanapata mafunzo ya
kuwaendesha viongozi hao.
Aidha amesema kuwa kwa sasa
wanaishauri Serikali kutoa waraka maalum utakaosaidia kuwadhibiti
viongozi ambao wanatoa maelekezo kwa madereva wakimbize magari kwa
mwendokasi na malengo ya baraza hilo ni kuimarisha utendaji wa kamati za
usalama za mikoa na kuweka mikakati ya pamoja ya utendaji na usimamiaji
wa majukumu ya kamati hizo.
“Kudhibiti mwendokasi na kuovateki
kunakofanywa na madereva wa magari kwa kuwakamata,kuwaweka mahabusu na
kuwaondolea sifa za madaraja C na E kwenye leseni zao hivyo kukosa sifa
ya kuondesha magari hayo,”amesema Masauni
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari na wajumbe wa Baraza hilo, ambapo aliwataka madereva wa magari ya Serikali kufuata sheria za barabarani na atakaye vunja sheria hizo atakamatwa, atawekwa mahabusu, kuwapeleka mahakamani pamoja na kuwaondolea sifa za madaraja C na E kwenye leseni zao na hivyo na hivyo kukosa sifa za kuendesha magari hayo. Kushoto meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, jana.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari na wajumbe wa Baraza hilo, ambapo aliwataka madereva wa magari ya Serikali kufuata sheria za barabarani na atakaye vunja sheria hizo atakamatwa, atawekwa mahabusu, kuwapeleka mahakamani pamoja na kuwaondolea sifa za madaraja C na E kwenye leseni zao na hivyo na hivyo kukosa sifa za kuendesha magari hayo. Kushoto meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, jana.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...