Na Humphrey Shao, Muheza Tanga
MSANII wa Muziki wa Kughani , Mrisho Mpoto alimaharufu kama Mjomba amesema kuwa kampeni ya Nyumba ni Choo inayoendelea katika Wilaya ya Muheza imeweza kuja na Matokeo mazuri ya awali kwa wakazi wa eneo hilo kuweka mahadhimio ya kujenga vyoo bora.

Mrisho Mpoto amesema kuwa wakati wanafika katika Wilaya hiyo walijua itakuwa ni ngumu lakini cha ajabu wakati wanatoa somo la kwanza tu wakazi hao wamehazimia kujengwa vyoo kabla ya kukamilika kwa mradi.

"wakazi wa Muheza wamehazimia kujenga vyoo bora kwa kukubali kauli mbiu yetu kuwa nyumba ni choo hivyo kwasasa wanamiminika uwanjani kwa ajili ya kujifunza namna ya kujenga kuta nne za Choo Bora" amesema Mrisho .

Mpoto  amemaliza kwa kuwataka watanzania kuweka kipaumbele katika ujenzi wa vyoo bora ambavyo vitachangia kupunguza magonjwa ya kuambukiza yatokanayo na uchafu kama kuhara na kipindupindu
 Msanii wa Muziki wa Kughani, Mrisho Mpoto akitumbuiz akatika kampeni ya Nyumba ni Choo Katika Wilaya ya Wizara ya Afya Wilaya Muheza mkoani Tanga ambapo watu wameweza kuitikia wito wa kampeni hiyo na kujiwekea mahazimio ya kujenga vyoo bora kabla ya kukamilika kwa kampeni hiyo
 Wakazi wa Wilaya ya Muheza wakifatilia kampeni ya Nyumba ni Choo inayoendeshwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Mjomba Bendi
 Wacheza Sarakakasi wa kundi la Mjomba Theatre  wakionyesha mchezo wa Sarakasi wa kuhamasisha ujenzi wa Vyoo bora kwa kauli ya Nyumba ni Choo kwa wakazi wa Muheza.
Burudani ikiendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...