Na Kulwa Mwaibale

Hospitali ya Kimataifa ya Apollo yenye makao makuu yake nchini India, imetoa ofa ya matibabu kwa wanamuziki wa Tanzania.

Akizungumza mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, kwenye mkutano baina ya wawakilishili wa Hospitali ya Apollo nchini Tanzania pamoja na wanachama wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Parwez Audax alisema lengo la kutoa ofa hiyo ni kuhakikisha wanamuziki nchini wanakuwa na afya njema.

Audax alisema, baada ya kubaini watu wengi nchini wanasumbuliwa na maradhi hususan ya uvimbe kwenye kizazi kwa wanawake, tezi dume, saratani ya ini pamoja na magonjwa ya mgongo na uti wa mgongo wameamua kutoa ofa ya matibabu kwa gharama nafuu kwa wanamuziki.

"Kwa kuanzia tumeamua kutoa ofa ya gharama nafuu kwenu wanamuziki kwa watakaojiunga na bima ya afya ya Apollo," alisema mwakilishi huyo.

Naye Dr Sandip Jhala ambaye ni miongoni mwa madaktari bingwa wanaotibu bila kufanya upasuaji wa Hospitali ya Apollo, alisema baada ya kuona watu wengi kutoka nchi za Afrika wanasumbuliwa na uvimbe kwenye kizazi, tezi dume na magonjwa mengine aliamua kuja Afrika kutoa tiba.

"Nilipoona watu wengi kutoka Afrika hususan Tanzania wanakuja kwenye hospitali yetu ya Apollo India kutibiwa niliamua kuja kufanya utafiti kujua ukubwa wa tatizo na kutoa tiba," alisema Jhala.Dr. Jhala alisema matibabu ya kuondoa uvimbe katika kizazi kwa wanawake bila ya kufanya upasuaji hayahitaji nusu kaputi na mgonjwa hutumia siku mbili tu kukaa hospitali na anakuwa na asilimia 33 mpaka 53 ya kupata mtoto.
Daktari Bingwa wa kutibu bila ya kufanya upasuaji kutoka Hospitali ya Apollo, Dr Sandip Jhala akielezea namna wanavyofanya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye kizazi, tezi dume na magonjwa mengine katika mkutano uliowakutanisha Wanaumoja wa Wanamuziki Tanzani (TAMUFO) pamoja na wawakilishi wa Hospitali ya Apollo hapa nchini mkutano uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Rais wa TAMUFO, Dkt. Donald Kisanga akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwanamuziki Kasim Salehe Mafanya, akiwa na mwanamuziki wa nyimbo za injili katika mkutano huo.
Viongozi wa TAMUFO na wadau wa muziki wakiwa meza kuu. 
Lina Munisi aliyetolewa uvimbe na Dr.Jhala bila ya kupasuliwa katika Hospilati ya Apollo nchini India akitoa ushuhuda wake kwa wanamuziki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...