NCHINI India Jyoti Kisanji Amge aliyezaliwa mwaka 1993 imethibitika kuwa ndiye mwanamke mfupi zaidi anayeishi na makazi yake ni huko Nagpur nchini India.

Akizungumza na jarida la Wider World Ranjana ambaye ni mama mzazi wa Jyoti amesema kuwa binti yake huyo alionekana na matatizo hayo alipofika miaka 5 na kwa mujibu wa madaktari walisema kuwa na tatizo la dwarfism linalofahamika kama achondroplasia na wakathibitisha kuwa kimo chake hakiwezi kuongezeka.

Jyoti alivuma sana mwaka 2009 alipoonekana kwenye televisheni ya Fuji ambapo katika kipindi hicho alipimwa na kugundulika kuwa na futi 2 pekee na ikathibitika kuwa ni mwanamke pekee anayeishi na wakati huo alikuwa na miaka 15 na alieleza kuvutiwa kwake na masuala ya urembo na alieleza kuwa ana ndoto za kuja kuwa muigizaji.

Hadi kufika Desemba 2011 alipofikisha miaka 18 historia yake ilizidi kukua na kuwa mwanamke mfupi zaidi anayeishi.

Amehudhuria matamasha mbalimbali na kukutana na aliyekuwa mwanaume mfupi zaidi duniani Chandra Dangi na amewahi kutokea katika wimbo wa Bhangra Singh na katika makala ya Bodyshock iliyojulikana kama Two Foot Tall Teen.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...