Anaandika Mh.Jumaa Hamidu Aweso .

“Ndugu zangu ,nina furaha sana huenda zaidi ya siku zote ukitoa siku niliopata ridhaa ya kuaminiwa na wana Pangani kua Mbunge wao.

Asanteni sana, Kitu kinachoifanya siku hii ya leo kua ya kipekee sana ni BARABARA yetu ya PANGANI kupewa kibali rasmi cha matengenezo toka kwa Mh.Raisi wetu Mpendwa Dk.John Pombe Magufuli na hapa nimefika ofisini kwa Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu Dodoma kujionea na kushukuru. 

Ndugu zangu kila kilio kina mwenye ,;machozi ya furaha yamenitoka nilipopewa habari hizi,nimekumbuka mbali sana tulivyoumia, tulivyoteseka pamoja na kwa miaka mingi sana kusubiri hili. 

Hisia zimenipeleka mbali nilivokosa amani toka nilipopata ridhaa ya kua Mbunge namna nimekosa usingizi kila nikiwaza kulimaliza na kufanikisha hili,nilifikia hatua kila nikisimama Bungeni nasemea barabara tu,nilipiga mpaka MAGOTI kwa Waziri Mbalawa alipofika Pangani,nimeenda ofisi zote hamna sehemu sijafika kuisemea barabara hii,nimetembelea Media mbalimbali.,nimemuomba sana Mungu kila nifapo Dua.! 

 Leo ni siku ya kihistoria ninaomba kuwajulisha rasmi kua tunaenda kupata barabara ya kiwango cha lami na zoezi hili litaanza muda si mrefu. Tumesema sana,tumepaza sauti kila kona,tumezungumza na kila aliehusika na sasa faraja kubwa hii hapa Mbele yetu.! .

 Nichukue nafasi hii kuwashukuru sana wana Pangani kwa uvumilivu wenu kipindi chote nilipowaambia naipambania barabara hii,na niwaombe tuendelee kua na subira mpaka mchakato unapoanza,nawashukuru sana kwa Dua zenu na nawaomba uzidi kuniombea nina mengi ya kufanya kwa ajili yenu. 

 Aidha nimshukuru Mkuu Wa Wilaya Pangani Mh.Zainab,Mkuu wa Mkoa Mh Shigela alielibeba hili kutusaidia na zaidi Waziri wa Uchukuzi,Miundombinu na Mawasiliano MhKamwele kwa kazi kubwa waliofanya kunipa sapoti katika hili pasina kumsahau mtangulizi wake Mh.Mbalawa. 

 Mwisho nikiri nimeupokea utendaji wa Mh.Raisi wetu wa Miaka mitatu kwa moyo wa furaha sana na Mungu ampe nguvu na Afya na maisha marefu tokana na hiki kilio cha muda mrefu kinachokwenda kufutika ikiwa ni kama Pangani tulikua pangoni sasa tunaenda kupaa angani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...