Waziri Mkuu Mstaafu
Edward Lowassa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ya
mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi, utakaofanyika Disemba 2, 2018
katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT)-Sinza Mapambano, jijini
Dar es Salaam.
Mbali na Lowassa,
waimbaji watakaosindikiza uzinduzi wa albamu hiyo inayoitwa ‘Hakimu wa Haki’ ni
Bahati Bukuku, Dk Tumaini Msowoya, Tumaini Njole, Tumaini Mbembela,
Madamu Ruth ,Iren Mwamfupe, Bony Mwaitege, Margie Muliri, Juvenalista
Mabuma Edson Mwasabwite.
Akizungumza na
Mwananchi, Mariam alisema amemualika Lowassa kwa sababu ndiyo aliyeanza kuibu
kipaji chake, alipompa nafasi ya kuimba siku ya sherehe yake ya kuzaliwa.“Lowassa ni baba yangu,
aliibua kipaji change ndio maana nikatamani awe mgeni rasmi na amekubali,
namshukuru sana Mungu kwa sababu hii,” alisema.
Alitaja nyimbo zilizo
kwenye albamu yake kuwa ni Hakimu wa Haki, Pam Pam tukuza, Natafuta Mshauri,
Chereko leo, Nasikia Kuitwa, Agano Langu, Ushindi Lazima na Mapambazuko.“Nasikia kuitwa ndio
wimbo ambao niliimba wakati nikianza mbele ya baba Lowassa, kwa hiyo ilipofika
hatua ya kuandaa albamu yangu niliuweka na huo kwa sababu ndio ulionifungulia
njia,” alisema.
Akizungumzia changamoto
alizokutana nazo kwenye muziki huo, Mariam alisema ni gharama kubwa ya uandaaji
wa muziki pamoja na kusambaza kazi hiyo.“Naimba muziki kwa
sababu nasikia kuitwa kwa ajili ya kazi hiyo, kusema kweli gharama za uandaaji
wa kazi nzuri ni kubwa hata hivyo namshukuru Mungu kwa sababu nimeshakamilisha
hatua ya kwanza,” alisisitiza.Mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi ambaye atazindua albamu yake skiku ya tarehe 2 mwezi wa 12 mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...