WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewaagiza Warajisi Wasaidizi wa Ushirika katika Mikoa yote inayolima korosho nchini waandae semina kwa Maafisa Ushirika, viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS), maafisa ugani na wakulima ili kuwawezesha kubaini na kupanga korosho katika madaraja kuanzia ngazi ya vyama vya msingi.
Amesema jambo hilo litasaidia mkulima aweze kujua korosho aliyoipeleka ina ubora gani akiwa huko kijijini na wanapoifikisha kwenye ghala kuu wafanye kazi ya kuthibitisha , kwa hatua hiyo itasaidia kuondoa malalamiko kuhusu madaraja . 
“Zoezi hili licha ya kuthibitisha ubora itasaidia kuboresha uzalishaji kwani wakulima wataelimishwa namna ya kuimarisha na kuboresha uzalishaji wa korosho nchini ikiwa ni pamoja na matumizi bora ya viatilifu ’’
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Novemba 21, 2018) wakati alipotembelea kiwanda cha korosho cha BUKO kilichopo kwenye Manispaa ya Lindi, ambapo ameshuhudia korosho zikipimwa ubora kwenye ghala kuu lilipo kiwandani hapo.
Ameagiza semina ifanyike mwakani ili maafisa ushirika baada ya kupata mafunzo wawasaidie wakulima kwenye msimu ujao watambue korosho walizopeleka kuziuza zina ubora gani. 
Waziri Mkuu amesema katika semina hiyo wakutane maafisa kilimo na maafisa ushirika ili wapate taaluma hiyo itakayowawezesha kupima korosho na kuitenga katika madaraja na kuwaondolea shida wakati wa mauzo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua uwanja wa michezo wa Ilulu uliopo mjini Lindi, Novemba 21, 2018.  Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua uwanja wa michezo wa Ilulu uliopo mjini Lindi, Novemba 21, 2018.  Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha korosho BUKO  cha mjini Lindi ambacho kimesimamisha uzalishaji, Novemba 21, 2018.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua  magunia ya korosho yaliyohifadhiwa kwenye ghala la kiwanda cha korosho cha BUKO cha mjini Lindi wakati alipotembelea kiwanda hicho, Novemba 21, 2018.  Kushoto ni Mkurugenzi wa  Kampuni ya Namgongo Holding iliyopewa dhamana ya kutunza ghala hilo, Ramadhani Katau. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati ,   Afisa anayesimamia Ubora wa Korosho, Dastan Milazi alipokuwa akipima korosho zilizopokelewa kwenye ghala la kiwanda cha korosho cha BUKO cha mjini Lindi wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichosimamisha uzalishaji, Novemba 21, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...