WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamesema Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu katika kusimamia matumizi endelevu ya maji ya Mto Nile kwa ustawi wa kiuchumi wa nchi zote.
Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 22, 2018) wakati akifungua mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Bonde la Mto Nile zilizopo Ukanda wa Maziwa Makuu uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.
Amesema nchi wanachama hazina budi kuimarisha ushirikiano ili ziweze kusimamia vizuri matumizi endelevu ya maji ya Mto Nile pamoja na kushughulikia changamoto zinazolikabili Bonde la Mto Nile. 
Waziri Mkuu ametaja baadhi ya changamoto zinazolikabili Bonde la Mto Nile kuwa ni pamoja na kushindwa kufikia makubaliano ya kuanzisha Kamisheni ya Kudumu ya Bonde la Mto Nile. “Kwa takribani miaka 10 sasa tumeshindwa kufikia makubaliano.”
Amesema, sambamba na changamoto hiyo nchi wanachama zimekuwa zikichelewa sana kutoa michango yao ili kuziwezesha taasisi zao kutekeleza ipasavyo majukumu yao, jambo ambalo si tu linachelewesha maendeleo bali linatishia usalama wa maji katika Bonde la Mto Nile.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu ametoa mapendekezo mbalimbali ili kuhakikisha kunakuwa na matumizi endelevu ya rasilimali za maji kwenye Bonde la Mto Nile pamoja na kusaidia nchi wanachama kupata maendeleo.

Moja ya mapendekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu ni pamoja na nchi wanachama kutoa elimu kwa wananchi wake kuhusu matumizi sahihi ya maji na umuhimu wa kutunza vyanzo vyake ili kuhakikisha kunakuwepo na matumizi endelevu ya maji.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri  la Nchi za Bonde la Mto Nile za Ukanda wa Maziwa Makuu kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Novemba  22, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa wakati alipowasili kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri  la Nchi za Bonde la Mto Nile za Ukanda wa Maziwa Makuu kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Novemba 22, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Bw. George Lugomela (kulia) kuhusu mashine ya kutambua uwepo wa maji ardhini  kabla ya kufungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Bonde la Mto Nile za Ukanda wa Maziwa Makuu kwenye hoteli ya Serena, Novemba 22, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama burudani ya ngoma  wakati alipowasili kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri  la Nchi za Bonde la Mto Nile za Ukanda wa Maziwa Makuu, Novemba 22, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Maji, Profesa Mbarawa Makame na watatu kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano  wa Afrika ya Mashariki,  Balozi Dkt.  Augustine Mahiga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...