Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog,Dodoma 

Spika wa Bunge Job Ndugai amewataka wabunge Bunge la Vijana, kutumia mafunzo ya Bunge hilo kwa weledi wa kutosha juu ya uendeshaji wa Bunge na kuwa mabalozi wazuri watakaporejea vyuoni.

Spika ameyasema leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa Bunge la Tano la Vijana ukiwa na lengo la kuwaandaa Vijana kuwa viongozi bora wa baadaye lakini pia kuwa na mijadala inayofika mwisho bila kugombana.Mkutano Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na UNDP kupitia mradi wa kuwajengea uwezo wabunge awamu ya pili (LSP II) na kufanyika katika ukumbini wa Pius Msekwa.

Spika amesema kuwa mkutano wa Bunge hili ambao umejumuisha vijana kutoka Vyuo vya Elimu ya juu , lina lengo la kuwawezesha Vijana hao kutumia mijadala zaidi na viongozi wao wawapo vyuoni badala ya kukimbilia migomo katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili.

Aidha Spika amebainisha kuwa, shabaha ya Bunge hilo ni kuwawezesha vijana kuelewa taratibu za uendeshaji wa Bunge,kuwafundisha Vijana Utamaduni wa kuvumiliana kwa kubishana kwa hoja na kuheshimu wengine kuwaelimisha Vijana juu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Jamii na Taifa kwa ujumla na kuwafundisha vijana umuhimu wa kufikia maamuzi baada ya mjadala wa pamoja.

Spika amewaomba wabunge kutumia mafunzo ya Bunge hilo kuwa na weledi wa kutosha juu ya uendeshaji wa Bunge na kuwataka kuwa mabalozi wazuri watakaporejea vyuoni. Akimkaribisha Ndugai, Spika wa Bunge hilo Zephania Sane amesema kuwa matarajio yao ni kujifunza jinsi Bunge linavyofanya kazi hususan ya kupitisha miswada na kutungwa Sheria za Nchi.Mhe.Sane amesema kuwa Vijana wapo pamoja na Rais John Magufuli na wanamuunga katika kila anachokifanya kwa mustakabali wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Bunge hilo ambalo linafanyika kwa muda wa siku tano, limejumuisha Vijana 60 kutoka Vyuo vya Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP),Chuo Kikuu cha Dodoma,Chuo cha Biashara Tawi la Dodoma (CBE) Chuo Kikuu cha Mzumbe,Chuo Kikuu cha Kiislam cha Morogoro na Chuo Kikuu cha Uhasibu Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Bunge la Vijana mwaka 2018 linalofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma kulia kwake ni Spika wa Bunge la Vijana Mhe. Zephania Sane na kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Ashiruna Mhunzi 
Mapambe wa Bunge akiongoza msafara wa Spika wa Bunge la Vijana kuingia Ukumbini kwa ajili ya kuanza Kikao cha Kwanza cha Bunge hilo kwa mwaka 2018 kilichofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. 
Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Zephania Sane akiapa kushika nafasi hiyo mbele ya Katibu wa Bunge hilo, Ndugu Alphonsina Ambrosi. Mkutano wa Bunge la Vijana mwaka 2018 unaendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Vijana mwaka 2018 wa wakila kiapo cha utii mbele ya Spika wa Bunge hilo la vijana, Mhe. Zaphania Sane.wengine ni Makatibu Kamati wa Bunge hilo.

Spika wa Bunge wa Bunge , Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Spika wa Bunge la Vijana mwaka 2018 Mhe. Zephania Sane kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge hilo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Mhe. Ndugai alikuwa mgeni ramsi na alifungua Bunge hilo la Vijana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...