Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

TAASISI ya Uongozi nchini (Uongozi Institute) imefanya kongamano lenye mlengo wa kukuza na kuimarisha uongozi na viongozi nchini hasa katika kutekeleza majukumu yao katika sekta wanazohudumia.

Akimwakilisha  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora George Mkuchika wakati  wa uzinduzi wa kongamano hilo  mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Uongozi Prof. Penina Mlama amesema kuwa lengo la kufanya kongamano hilo ni  kubadilishana mawazo kuhusu kukuza na kuimarisha masuala ya uongozi na viongozi nchini hasa katika utendaji.

Ameeleza kuwa mawazo yatakayotolewa katika mjadala huo yatumike katika kuboresha uongozi serikalini na katika sekta binafsi na yaendelezwe ili kuwawezesha viongozi kutenda kazi kwa kuzingatia misingi bora zaidi.Aidha ameeleza  Serikali iliona tatizo katika masuala ya uongozi na ilipofika mwaka 2010 Serikali ilianzisha Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) ili kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika utekelezaji wao wa majukumu.

Mlama amesema kuwa Serikali ya Awamu tano imedhamiria katika kuhakikisha viongozi wanafanya kazi kwa kuzingatia mihimili na maadili kwa ujumla na amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli amesimamia kwa kiasi kikubwa masuala ya uadilifu, nidhamu katika matumizi ya fedha za umma, maadili sehemu za kazi na kupiga vita vitendo vya rushwa na ufisadi.

Kwa upande wake  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja amesema kuwa kongamano hilo ni la kubadilishana mawazo kuhusiana na ukuzaji na uimarishaji wa uongozi na viongozi nchini na washiriki wametoka katika sekta mbalimbali ikiwemo Serikalini, Bungeni, Jeshini, vyama vya siasa na dini.Semboja amesema kuwa kongamano hilo ni la kupanga mikakati na sio kutathimini mifumo iliyopita na ya sasa. Na ameeleza kuwa watatathimini mifumo ili kujenga matokeo bora hapo baadaye.

Amesema kuwa historia inaonesha kuwa viongozi wanaofanya vizuri wanajengwa kutokana na mazingira ambayo watakuja kuongoza na wao kama taasisi watahakikisha wanasimamia majukumu hayo kikamilifu kwa kuandaa mijadala na makongamano mbalimbali yanayolenga kukuza na kuimarisha masuala ya uongozi na viongozi nchini.
 Mwandishi na mhadhiri Profesa Issa Shivji (kushoto) na Shekh mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Alhadi Mussa Salum (kulia) wakifuatilia mjadala huo uliolenga kukuza na kuimarisha uongozi na viongozi nchini.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja akihutubia wakati wa kongamano hilo ambapo ameeleza kuwa Taasisi hiyo itaendelea kuandaa mijadala na mada mbalimbali katika kukuza na kuimarisha uongozi na viongozi nchini.
 Mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Uongozi Prof. Penina Mlama akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa kongamano lililokuwa na mlengo wa kukuza na kuimarisha uongozi na viongozi nchini lililofanyika leo jijini Dar es salaam.
Aliyekuwa Spika wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda (kushoto) na aliyekuwa Waziri wa fedha Zakia Meghji wakifuatilia mjadala huo uliokuwa ukiongozwa  prof. Issa Shivji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...