Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

KAMPUNI ya Vodacom kwa kishirikiana na benki ya Commercial Bank of Afrika (CBA) wametangaza rasmi kampeni ya shinda na M -pawa itakayowasaidia wateja kujishindia zawadi kemkem.

Akimwakilisha Mkurugenzi wa benki ya CBA, Mkuu wa kitengo cha masoko wa benki hiyo Julius Konyani amesema kuwa wateja watakaoweka amana, kukopa na kulipa kwa wakati ndani ya wiki 6 kuanzia Novemba 1 watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali. 

Amesema kuwa wateja 200 watakaopatika ndani ya wiki 6 ambao huweka amana katika akaunti zao za M-pawa watashinda mara mbili ya amana walizoweka.Aidha amesema kuwa wateja 15 wanaokopa na kulipa kwa wakati watazawadiwa kiasi cha shilingi laki moja na kwa wiki 6 jumla ya wateja 96 watanufaika na zawadi hizo.

Konyani amesema kuwa droo kubwa itakayochezeshwa mwishoni kabisa jumla ya zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 100 zitatolewa, na hizo ni pamoja na bajaji tano zitakazotolewa kwa wateja watano ambao hukopa na kulipa kwa wakati kupitia M-pawa na mteja wa jumla atapata zawadi nono ya shilingi milioni 10.

Kwa upande wake Meneja masoko wa kampuni ya Vodacom Noel Mazoya amesema kuwa wao na washirika wao ambao ni benki ya CBA wataendelea kuleta karibu huduma za kijamii kwa mfumo wa kidigitali.Amesema kuwa hadi sasa wamewafikia zaidi ya wateja milioni 7 ambao wanatumia huduma ya Mpawa katika kuweka faida na kukopa na kwa usalama zaidi.

Mazoya amesema kuwa wateja wa Vodacom waendelee kutumia huduma hiyo ili waweze kunufaika na zawadi zinazotolewa na kampuni hiyo.
Meneja Masoko wa Vodacom,Noel Mazoya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wateja wa mtandao huo waendele kutumia ili waweze kunufaika na zawadi zinazotolewa.kulia ni Mwakilishi wa Meneja wa CBA,Julius Konyani (Picha na Emmanuel Massaka MMG).
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa CBA,Julius Konyani wa (kwanza kulia) akishangilia mara baada ya kupatikana ya mshindi katika droo iliyochezeshwa leo jiji Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...