Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kufanya uchambuzi na kuwakagua wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika benki zote nchini.

Hayo yamesemwa na Gavana wa Benki Kuu Profesa Florens Luoga wakati akifunga semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi iliyoandaliwa na BoT Mjini Dodoma Profesa Luoga amesema uamuzi huo unalenga kulinda fedha za wananchi ambazo wameweka benki pamoja na kuondoa wafanyakazi wasio waaminifu.

"Benki Kuu tunao mkakati wa kuhakikisha tunafanya ukaguzi ambao lengo lake litakuwa kuhakikisha wanapatikana wafanyakazi waliowaamini na wenye uwezo wa kulinda fedha za wateja.Tunahitaji kuona wafanyakazi wa benki ambao wanatambua na kuheshimu misingi ya kaziza benki,"amesema Profesa Luoga na kuongeza ni muhimu kwa BoT kulinda za wateja.

Amefafanua siku za nyuma kulikuwa na baadhi ya fedha za wateja wadogo zilizohifadhiwa kwenye baadhi ya benki, ziliibwa kwa ujanja na wafanyakazi wa benki hizo jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Ameongeza kiongozi mzuri wa benki lazima awe mwaminifu na ndio maana BoT wanataka kuhakiki wafanyakazi wa benki zote nchini.

Amefafanua huu ni wakati wa kuwa na wafanyakazi wa benki amabo ni sahihi kwa kazi hiyo, hivyo kupitia uchambuz wa kina ambao utafanyika watabaini wafanyakazi waliopo na uwezo wao na waamini kazini.

Profesa Luoga ameeleza namna ambavyo kuna baadhi ya wateja wa benki ambao si waaminifu walivyokuwa wanatengeneza mazingira ya kujipatia fedha ambapo walikuwa tayari kutafuta watu na kuwajazia fomu na kisha kuwapatia mkopo.

"Anakuja mfanyakazi wa benki fulani anakwambia fungua akaunti ili upate mkopo, baadae anakupa mkopo wa Sh.milioni 50 halafu yeye anachukua Sh.milioni 20 na kukuachia Sh.milioni 30.Lazima ifike wakati tuwe na wafanyakazi waamini katika sekta ya kibenki,"amesema. Amesema BoT imejipanga kwa kila hali kuhakikisha inalinda haki za wateja ikiwamo kulinda fedha zao kwenye benki huku akieleza kuwa wanataka huduma za kifedha zimfikie mwananchi kila mahali na bila kikwazo.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Profesa Florens Luoga akizungumza na waandishi wa habari za fedha na uchumi wakati akifunga mafunzo yaliyoandaliwa na BoT kwa waandishi hao
 Mtunza Muda katika mafunzo ya semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi Bakari Kimwanga(aliyesimama) akitoa shukrani kwa Gavana wa BoT pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo kwa kuandaa mafunzo ya habari za fedha na uchumi
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga akiwa ameshikana mkono na Mwakilishi wa Michuzi Blog Said Mwishehe baada ya kufunga mafunzo ya uandishi wa habari za fedha na uchumi iliyofanyika BoT tawi la Dodoma.Wanaoshuhudia ni sehemu ya maofisa wa benki hiyo na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...