Na Mwadishi wetu, Morogoro
NAIBU Waziri wa Madini, Doto Biteko ameiagiza Menajimenti ya Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji ch  Mangae  wilayani Mvomero, mkoani Morogoro kusimamisha uchimbaji  hadi itakapokamilisha taratibu za kisheria za Serikali  zinazosimamia madini  pamoja na kuwalipa fidia wananchi waliohamishwa meneo yao  waliokuwa wakiishi.

Biteko alitoa agizo hilo baada ya kufanya ziara  ya kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo kwenye  eneo la mgodi huo uliopo katika vijiji vya Mtupule na Mangae  na  kubaini imekuwa ikeindelea kuchimba madini  ya dhahabu kinyume na sheria  licha ya kutakiwa kukamilisha kwanza  utaratibu waliopewa wa kisheria .

Mbali na hilo , Naibu Waziri alionya na kutoa wito  kwa Watanzania wote wanapoamua kuingia mikataba na mikataba ya  wachimbaji wadogo ni lazima itambuliwe na serikali kwa mujibu wa sheria ya uwekezaji  sekta ya madini na si vinginevyo.

Naibu Waziri alisema , kufuatwa kwa sheria na  utaratibu wa mikataba na wawekezaji wa n je inalenga kuwalinda   uwekezaji wao  ili  baadaye wasione wananyanyaswa pale  mikataba walioingia na watu wasio waaminifu inakinzana na sheria mpya  ya  madini

Hata hivyo alisema ,  manufaa ya madini kwa wananchi wa eneo hilo hayawezi kupatikana  endapo mahusiano kati ya mgodi na wananchi hayatakuwa mazuri na kwamba  rasilimali za nchi lazima ziwanufaishe Watanzania  wote yakiwemo Madini.
 Mkazi wa kijiji cha Mangae , kata ya Mangae, wilayani Mvomero mkoani Morogoro, Anita John  akitoa malalamiko yake  kwa Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko ( hayupo pichani )  kuhusu  Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa  dhahabu  katika eneo la kijiji hicho kuendesha shughili zao pasipo kuwafidia  makazi yao  waliyokuwa wakiishi kupisha uchimbaji wake.
 Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  akisoma  baadhi ya nyaraka za  Kampuni ya MMC  ya  uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae  wilayani Mvomero, mkoani Morogoro  wakati wa  ziara ya  kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo na ( wapili kulia) ni Mkuu wa wilaya hiyo, Mohamed Utaly.
 Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  ( aliyeweka mikono mfukoni) akipewa maelezo na kuangalia mashine  za  Kampuni ya MMC zilizofungwa kwenye mgodi wa uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae  wilayani Mvomero, mkoani Morogoro  wakati wa  ziara  ya kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo.
 Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  ( aliyeweka mikono mfukoni) akiteremka chini kutoka kuangalia mashine  za  Kampuni ya MMC zilizofungwa kwenye mgodi wa uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae  wilayani Mvomero, mkoani Morogoro   wakati wa ziara  ya kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...