NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO

MKUU wa wilaya ya Bagamoyo ,Mkoani Pwani ,Zainabu Kawawa ameagiza 
watumishi wa idara ya fedha wanaoshughulika na ukusanyaji mapato katika halmashauri ya Chalinze, wakamatwe ili kupisha uchunguzi na watakapobainika kusababisha upotevu wa mapato hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Amefikia hatua hiyo, kufuatia hali ya ukusanyaji mapato katika halmashauri hiyo kuwa chini ya kiwango ,kutoka wastani wa sh. milioni 950 kwa mwezi na kushuka hadi milioni 550-659 .#

Zainabu alitoa agizo hilo ,wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo.Aliwataja wahusika hao kuwa ni pamoja na mweka hazina David Rubibira na wahasibu watatu ambao ni Waziri Ally,Jumanne Sanga na Maneno Kwambwa,ili kupisha uchunguzi .

Zainab alisikitishwa na ukusanyaji mapato kwa kudai kuna mianya ya ubadhirifu wa mapato kwani mapato yakikusanywa kwa umakini yanafikia sh. milioni 920 kwa mwezi kwa chanzo cha madini ya kokoto nje ya vyanzo vingine kwa maana ya sh. milioni 33 kwa siku.

Hata hivyo ,kutokana na makisio hayo Zainab aliondoa imani na mapato yanayokusanywa katika halmashauri hiyo ambayo ni wastani wa milioni 550 hadi 659 kwa mwezi.Katika kikao hicho alimtaka mkuu wa polisi Chalinze kuwaweka chini ya ulinzi na kuwachukua kwa ajili ya uchunguzi .

"Nimekuwa nikifuatilia ukusanyaji mapato kuna mianya mingi ya utoroshaji mapato, tusitafutane wala kujaribiana kwa kuvujisha mapato tumepoteza mapato sana kwenye makrasha kwa siku tuna uwezo wa kukusanya milioni 33 ,kwa mwezi tuna uwezo wa kukusanya zaidi ya milioni 900"

"Badala ya kufuatilia na kukagua mnakaa ofisini ,katika hili hatuwezi kuvumiliana hata kidogo,,"mkurugenzi nakuagiza watumishi wanaohusika na mapato wakae pembeni kwa hatua zaidi kuanzia leo .Zainab alisisitiza , vyombo vya usalama vifanye kazi katika kuchunguza suala hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...