Na Editha Shija -Tabora

MKUU wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora Godfrey Ngupula amewaagiza wataalamu wa kilimo wote waliopo katika wilaya hiyo kwenda vijijini kwa ajili ya kuwapa wakulima elimu ya kilimo bora na mbegu imara zinazofaa katika kipindi hiki cha kilimo.

Akizungumza na Michuzi Blog ofisini kwake jana Ngupula amesema mtaalamu atakayekutwa ofisini atakiona cha moto kwani huu wakati si wa kumuuacha mkulima aendelee kufanya kilimo cha mazoea na kisichokuwa na tija bali kimnufaishe mkulima na maisha yake.

Amesema kuwa kipindi hiki cha mvua ambapo maandalizi ya kilimo ndio yanaanza wataalamu wa kilimo hawapaswi kukaa maofisini kwani ni wakati wa kuhamishia ofisi zao mashambani na siyo mjini huku akiwataka maofisa tarafa na watendaji wote na vijiji na kata kushirikiana kwa karibu zaidi na wataalamu wa kilimo ili kuhakikisha wakulima wanapata elimu 
itakayowasaidia kuongeza uzalishaji mkubwa wa mazao.

Sambamba na hayo mkuu huyo amemalizia kwa kufafanua kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa na kwamba kitasimamiwa vizuri na wakulima wakaelimishwa ipasavyo na kuachana na kilimo kisichokuwa bora,kwani maisha yao yatabadilika na Mapato ya halmashauri yataongezeka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...