Na Baba Faisal
SHANGWE za kibabe zimetawala leo katika Mji wa Smbawanga mkoani Rukwa baada ya msanii mwenye nyota yake ya kupendwa na anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa sasa Naseeb Abdull a.k.a Diamond kutua katika mji huo.
Diamond akiwa ameambatana na wasanii wengine kutoka lebo ya WCB wakiwa pamoja na wasanii wengine nchini wametua kwenye mji huo wa Sumbawanga kwa ajili ya kufanya tamasha la Wasafi Festival.Wakati msanii huyo anawasili mashabiki wa muziki wa kizazi kipya waliamua kujitokeza kwa wingi kumpokea.
Hivyo muda wote mashabiki walikuwa wakipaza sauti zao zilizoambatana na shangwe la aina yake wakiimba "Simbaa...Simba...Simba ...Simba..."wakiwa na maana ya kumuita Diamond ambaye huwa anapenda kujiita Simba.Diamond ameenda Sumbawanga kwa akiwa na ndege ndogo ya kukodi ambapo kabla ya kushuka mshabiki wa burudani waliamua kuizunguka ndege hiyo na kisha wakishangilia kwa sauti ya juu.
Hata hivyo Diamond alikuwa wa mwisho kushuka ndani ya ndege hiyo ambapo mbali ya shangwe kutawala wapo mashabiki walioona isiwe tabu bwana, hivyo walichukua simu zao na kisha kuanza kupiga selfie.Baada ya kutua kwenye mji huo kikubwa ambacho mashabiki wa burudani wanakisubiri ni kumuona Diamond akiwa jukwaani akiwapagawisha kwa nyimbo zake mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...