Katika kuungana na juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mh. Rais Dkt John Pombe Magufuli, Shirika la Digital Pipeline UK, kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia wameanzisha mradi mkubwa utakaobadilisha na kuboresha utoaji wa elimu nchini kuanzia shule za msingi za serikali hadi kidato cha sita kwa njia ya mtandao salama (Secured School Network) utakaobeba mtaala (curriculum) na vitabu vya maarifa mbalimbali vinavyokwenda na wakati ili kuwafanya walimu na wanafunzi kujinoa ipasavyo na kuwa wabunifu wanaoweza kushindana katika ulimwengu wa maarifa kwa wakati. (Communication Tool).
Hayo yameelezwa jijini Kent nchini Uingereza leo, tarehe 12/12/18 na Ndugu Abraham Sangiwa, Mkurugenzi na Mwenyekiti wa DIGITAL PIPELINE UK ambayo inafadhiliwa na Bill and Melinda Gate Foundation, Metropolitan Police UK, National Health Services UK and Vauxhall Motors UK, Katika hafla iliyofanyika katika ofisi kuu Priory Park jijini Kent nchini Uingereza
Uzinduzi huo pia ulishuhudiwa na wadau mabalimbali akiwemo Deputy Lieutenant of Kent Trevor Sturgess, Bevil Williams C.E.O at Digital Pipeline, board members, wafanyakazi wa Digital Pipeline UK na wadau mbalimbali
Ndugu Abraham Sangiwa aliendelea kusema napenda kuishukuru wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia kwa kuniteua kuwa Balozi wa Wizara katika Mradi huu wa Digital Campus in Tanzania, haikuwa kazi rahisi kufanikisha mradi huu kwa Tanzania kwani Digital Pipeline UK inafanya shughuli zake katika nchi zaidi ya ishirini na saba barani Afrika, nchi nane bara la Asia, baadhi ya nchi bara la  Ulaya, Amerika ya Kati na Kusini, na kila moja ilipenda mradi huu mkubwa wa kujenga Digital Campus Plant kubwa na ya pekee barani afrika unfanyike katika nchi zao, lakini kutokana na uzalendo na uelewa kwa timu nzima ya Wizara ya Elimu na viongozi wake na  kwa kuzingatia vigezo vilivyo wazi kwa serikali ya Tanzania vimesaidia kuleta mradi huu wenye manufaa makubwa nchini.

 Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi, Digital Pipeline UK (Computers 4 Africa) Ndugu Abraham Sangiwa (Kushoto), Bevil Williams C.EO.  Katikati ni Deputy Lieutenant of Kent Uingereza - Trevor Sturgess wakibadilishana mawazo katika ofisi kuu ya DP jijini Kent nchini Uingereza, wakati wa kushuhudia upakiaji wa vifaa vya kielektroniki kwa ajili ya mradi wa “Digital Campus on Education in Tanzania” utakaofanywa kwa pamoja na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia. 
Vifaa mbalimbali vya kielektroniki vikipakiwa kwenye container tayari kwa safari ya kuelekea Tanzania. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...