Na Hassan Silayo - MAELEZO

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas ameendelea na utaratibu wa kuwapigia simu Wakuu wa Taasisi ili kujibu hoja za wananchi moja kwa moja katika ziara yake kwa vyombo habari inayoendelea nchini.

Katika mahojiano na kituo cha Redio cha Jembe FM 93.7 mkoani Mwanza, 

Dkt. Abbasi alimpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA), Dkt. Irene Isaka , ambaye alifafanua kuhusu Sheria mpya ya Hifadhi ya jamii.Dkt. Irene alisema kuwa baada ya kuunganisha Mifuko mafao yamezidi kuboreshwa ili mstaafu awe anapokea fao kubwa la mwezi.

Dkt. Isaka amesema kuwa mstaafu atalipwa fao la mkupuo la 25% na baada ya hapo fao la mwezi litakuwa kubwa zaidi tofauti na ilivyokua awali ambapo fao la mkupuo lilikuwa kubwa lakini fao la kila mwezi likawa dogo kumfanya mstaafu ashindwe kumudu maisha.

Aidha, Mkurugenzi wa SSRA ametaja faida zingine za Sheria mpya kuwa ni familia ya mstaafu kuendelea kulipwa kwa miaka mitatu baada ya mstaafu kufariki, fao la kuachishwa kazi, kuweka usawa katika kulipa mafao na kuwa hivi sasa wanaweka utaratibu wafanyakazi wapate mikopo ya nyumba kupitia pensheni zao.

Katika mahojiano hayo ya moja kwa moja na Kituo cha Jembe FM, Dkt. Abbasi pia alimpigia simu Mkurugenzi wa Wakala wa Hufuma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamisi kujibu hoja na masuala ya usafiri wa maji hasa ununuzi w meli mpya Ziwa Victoria ulipofikia.

Bw. Hamisi alielezea vema hatua ambazo Serikali imechukua na inaendelea kuzichukua kuboresha usafiri wa majini.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali akifanya mahojiano maalum na kituo cha Radio cha Jembe Fm cha Jijini Mwanza kuhusu miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Jembe FM 93.7 mkoani Mwanza, Jimmy Kagaruki akisoma maswali yaliyokuwa yakitumwa na waskilizaji yaliyohusumiaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...