Na Bashir Yakub.
Huna haja ya kuvutana na mtu kuhusu iwapo wewe ni baba wa mtoto au hapana. Nimesema baba kwasababu wasiwasi wa aina hii mara zote upo kwa wanaume. Kuwa fulani ni mama wa fulani karibia mara zote hapana utata.

Basi wapo wanaopenda au ambao wangependa kufanya vipimo vya vinasaba(DNA) kuthibitisha kama ni wazazi kweli ama hapana. Nitaeleza utaratibu mzima hapa kutokana na Sheria ya Usimamizi wa Vinasaba vya Binadamu ya 2009,Sura ya 73.

1. NANI ANAWEZA KUPIMWA DNA.
Yeyote ambaye anahitaji kujua kuhusu uhalali wa uzazi wake anaweza kupima DNA. Upimaji huu hauna umri. Hata hivyo DNA si kwa jili ya masuala ya kuthbitisha uzazi tu, bali hutumika hata katika masuala ya ushahidi na upelelezi.

2. NANI ANA MAMLAKA YA KUOMBA DNA KUPIMWA.
Si kila mtu anaweza kuomba kupima DNA. Hata kama mwenye uhitaji ni wewe lakini bado huna mamlaka ya kuomba kupima DNA. Kifungu cha 25(2) cha Sheria niliyotaja hapo juu kinawataja wafuatao kuwa na mamlaka ya kuomba DNA kupimwa. Kinamtaja hakimu ambapo kuna kesi/shauri fulani linaendelea, Wakili, afisa ustawi wa jamii, afisa polisi mwenye cheo zaidi ya inspector,daktari, na mkuu wa wilaya.Hawa ndio wenye mamlaka(Requesting Authority).Kwahiyo wewe ukiwa na shida ya DNA unaweza kumuona mmoja kati ya hawa ili aandae maombi ya kupima DNA na kuyapeleka kunakostahili.

3. MAOMBI YA DNA YANAPELEKWA WAPI
Kifungu cha 24 cha Sheria ya Usimamizi wa Vinasaba kinaitaja maabara ya Vinasaba vya binadamu ya Mkemia Mkuu wa serikali kuwa na Mamlaka ya kupima DNA. Pia kinazitaja na maabara nyingine ambazo zitakuwa na leseni maalum ya kupima DNA kuwa na mamlaka hayo.

Kwahiyo maombi ya DNA yatapelekwa moja kati ya sehemu hizo mbili.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...