Na Ali Issa Maelezo Zanzibar

Jumla ya kinamama 1,339 wamejitokeza katika uchunguzi pamoja na kufanyiwa vipimo vya maradhi ya kensa ya shingo ya kizazi katika hospitali kuu ya mmanazi mmoja mjini Unguja.

Mratibu wa mradi wa uchunguzi wa kensa ya shingo ya kizazi,Dk. Omar Mwalimu Omar alitoa kakwim hiyo huko hospitali ya mnazi mmoja wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara maalum ya kutembelea eneo linalo endeshwa zoezi hilo. Amesema katika zoezi hilo lililoanza Jumatatu iliopita hadi leo (Jumatatu) watu 36 kati hao wametiliwa mashaka na kufikia maamuzi ya kuchukuliwa vinyama ili kuchunguzwa kwa hatua nyengine na baadaye yatatoka majibu rasm ya afya zao.

“Mara baada ya kuwafanyia uchunguzi mwengine na pindi tukibaini kuna mwenye maradhi hayo , tutaanza naye kwa kumpata tiba kwa kutumia dawa kwa mujibu wa taratibu za kitaalam”alisema Dk Omar. Naye mtaalamu wa magonjwa ya saratani katika hospitali ya mnazi maoja, Dk Abdalla Yussuf Mohamed alisema katika zoezi hilo wanachunguza vinasaba vyote vya akinamama hao ambavyo ni muhimu katika uchunguzi huo.

Mapema Naibu Spika Mgeni Hassan Juma alisema ni vyema wakaongezwa wataalamu wazalendo katika kupata kujifunza kutoka kwa watalamu wakichina waliopo. Aidha aliwapongeza akinamama hao waliojitokeza katika zoezi hilo na kuwataka waendelee kuwahamasisha wenzao ili zoezi hilo lifanikiwe kama lilivyokusudiwa.
Mratibu wa Mradi wa Uchukuzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi Zanzibar Dkt. Omar Mwalim Omar akimkaribisha Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma katika Tiba ya Uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi inayofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar. 
Mratibu wa Mradi wa Uchukuzi wa Saratani ya Singo ya Kizazi Zanzibar Omar Mwalim Omar akimuonyesha jambo Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma wakati alipowatembelea Madaktari wanaoendelea kutoa matibabu Hospitalini hapo. 
Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa Maabara Kibwana Omar Kibwana wakati alipotembelea Chumba hicho cha Maabara Hospitalini hapo (kulia) Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman. 
Mtaalamu wa Magonjwa ya Saratani ya Shingo ya Kizazi Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt. Abdalla Yusssuf Mohamed akimpatia maelezo Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...