WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Mhe. Isack Kamwelwe amesema Serikali ina mkakati wa kutunga sheria ya kuunganisha Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)na Kampuni ya Maendeleo ya Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO) ili kuunda Mamlaka ya usimamizi na uendeshaji wa Viwanja vya Ndege hapa nchini.

Waziri Kamwelwe alisema hayo alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAA katika Ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.

Aidha, Waziri Kamwelwe alisema lengo la kuunganisha TAA na KADCO ni kuwa na Mamlaka kamili ili isimamie Viwanja vya ndege na kuhudumia ndege zote pamoja na kusimamia biashara za kimkakati kama mafuta ya Ndege na utoaji huduma katika Viwanja vya Ndege. 

Kamwelwe alisema “mafuta ya ndege hayadhibitiwi kama zinavyodhibitiwa nishati nyingine na EWURA. Kwa nini huku kwenye ndege msimamizi asiwepo? sasa ili kudhibiti hili mtakuwa mnauza mafuta ninyi na hii ni baada tu ya kuwa Mamlaka kamili,” alihoji .

Akizungumzia Jengo la III la abiria alisema kunahitajika Watumishi zaidi ya 600 hivyo lazima Serikali iangalie wanahitajika Watumishi wa aina gani ili kuijenga TAA katika sura mpya.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bw, Richard Mayongela alipokuwa akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika ukumbi wa LAPF Dodoma mapema leo.
 Wajumbe mbalimbali wa Baraza Kuu la Wafanyakazi walipokuwa wakifuatilia kwa umakini hoja zilizokuwa mezani  katika Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe alipokuwa akifungua rasmi Mkutano wa 22 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF, Dodoma mapema leo.  

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (tatu kushoto) katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TAA (MAB)  Mhandisi Prof. Ninatubu Lema (pili kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa TAA Bw, Richard Mayongela (pili kulia) na Wajumbe mbalimbali  mara baada ya kufungua Mkutano wa 22  wa Baraza Kuu la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa LAPF , Dodoma mapema leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...