Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
Mkurugenzi Mtendaji wa LSF Kees Groenendijk amesema wananchi wengi wanashindwa kupata huduma za msaada kisheria kutokana na kukosa uelewa wa kupata watoa huduma za msaada wa Kisheria. Groenendijk ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya inayojulikana  kwa jina la "Siyo Tatizo" inayolenga  kuongeza ufahamu kwa jamii kuhusiana uwepo wa upatikanaji wa huduma za bure za msaada wa Kisheria , amesema jamii imezungukwa na matatizo yanayotokana na kukosa msaada wa kisheria na kufanya kukosa haki zao.

Groenendijk amesema Kampeni hiyo ni kuongeza ngumu  ya uelewa kwa jamii juu ya upatikanaji wa huduma ya bure za msaada wa kisheria zitolewazo na wasaidizi wa kisheria. "LSF Tanzania kwa dhati inalenga kuleta unafuu  zaidi  hasa kwa wanawake wenye hali ngumu  ambao haki zao za msingi zimepewa zikifinywa au kukosekana kutokana na sababu mbalimbali hali hiyo imechangiwa zaidi na ukosefu wa usaidizi wa kisheria" amesema Groenendijk. Amesema kuwa kampeni hiyo watawafikia wananchi wote katika kampeni hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa LSF Kees Groenendijk akizungumza na waandishi habari wakati wa uzinduzi wa Kampuni  ya Siyo Tatizo Tena ya upatikanaji wa huduma za bure za  msaada wa kisheria iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Miradi wa LSF Scholastica Tully akizungumza kuhusiana kampeni ya kutoa huduma kuhusiana na upatikanaji wa huduma za bure za msaada wa kisheria wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya inayojulikana  kwa jina la Siyo  iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Kampeni ya Huduma za bure za msaada wa kisheria Mwasiti Almas akizungumza kuhusiana na kutoa elimu ya upatikanaji wa huduma za bure za msaada wa kisheria katika uzinduzi wa LSF iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kampeni ya Huduma za bure za msaada wa kisheria Lameck Ditto 'Dogo Ditto' akizungumza jinsi atavyohamasisha kuhusiana na kampeni ya kutoa huduma za bure za msaada wa kisheria wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya inayojulikana  kwa jina la Siyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa LSF Kees Groenendijk(wa kwanza kulia) akipeana mkono na Balozi wa Kampeni ya Huduma za bure za msaada wa kisheria Mwasiti Almas wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya inayojulikana  kwa jina la Siyo  inayohusuUpatikanaji wa Huduma za bure za msaada wa kisheria iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Aiseee sasa hao jamaa sie tunawapata vipi?

    Mngeshare mawasiliano yao

    ReplyDelete
  2. Huduma za kisheria kupatikana bure ni kitu sijawahi kukutana nacho. Hii ni kitu chakujionea kwa kweli.

    ReplyDelete
  3. Tunashukuru sana aisee kwa jambo hili kwa sisi wa vijijini najua tumepata shida sana katika uporwaji wa ardhi kwa kuwa hatuna hela,nina imani kwa jambo hili litatusaidia sana na pongeza uongozi wote kwa kulileta jambo hili katika jamii yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...