MENEJA uhusiano wa Kampuni ya michezo ya kubashiri (SPORTPESA) Sabrina Msuya ameeleza mafanikio ya kampeni ya shinda zaidi na sportpesa kutoka Bajaji 100 kushindaniwa mpaka kufikia Bajaji 26 zilizobakia kwa sasa kutokana na mwitikio mkubwa kwa wabashiri mwaka huu.

“Kiukweli kabisa tunajivunia kama SportPesa, kwa kupitia promosheni hii tumefanikiwa kubadili maisha kwa Watanzania kupitia ushindi wao wa ubashiri wa matokeo amesema Msuya"

Pia ameeleza kuna Mabadiliko mengi kati ya hayo ni washindi wamenunua viwanja na wengine wamejenga nyumba kwa kupitia bajaj wanazoshinda kupitia promosheni hii inayoendelea na wengine wanawalipia ada watoto zao ambalo ndiyo jambo la msingi kuona watu wakiendelesha familia zao kupitia ubashiri wao.

Vilevile Promosheni hii inatoa ajira kwa Watanzania, kwani wapo baadhi ya washindi ni waajiriwa wanaposhinda bajaj wanawapa watu wawafanyie biashara, hivyo utaona ni jinsi gani hapo tumehusika katika kuajiri.Na washindi wa mwaka huu wametoka Mikoa ya Mara,Dar es salaam,Morogoro,Mwanza,Kigoma na Tanga ambao washindi wa mwaka jana walitokea Mkoa wa Kahama,Newala,Arusha.

Sportpesa imewasaidia Watanzania kujifunza mbinu za kufanya biashara kwani kabla ya kushinda bajaj hizo walikuwa hawafanyi biashara zozote, lakini wanaposhinda wanaanza kujifunza kufanya biashara kwa kupitia hizo bajaj.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...