Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amewataka watumishi wa ofisi yake kuwa mfano wa kuigwa na taasisi nyingine kiutendaji kwa kufanya kazi kwa bidii, maarifa, uadilifu na weledi ili kujenga misingi bora ya utumishi wa umma nchini. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ametoa maelekezo hayo leo wakati akizungumza na menejimenti ya ofisi yake, lengo likiwa ni kufahamiana na kupanga mkakati madhubuti wa utendaji kazi utakaoziwezesha taasisi za umma nchini kutoa huduma bora kwa umma. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wamepewa dhamana ya kuhakikisha utumishi wa umma unakuwa na tija na maslahi kwa maendeleo ya taifa hivyo hawana budi kutekeleza wajibu wao kikamilifu. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, watumishi wakifanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma iliyopo, malalamiko yasiyo ya lazima kwenye eneo la utumishi na utawala bora yatapungua kwa kiwango kikubwa. 

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, mtumishi wa umma anatakiwa kupimwa kwa utendaji kazi wake kwa matokea chanya ili atakapopanda daraja ajivunie utendaji kazi wake na kuongeza kuwa, upimaji huo utapunguza malalamiko ya kutopandishwa madaraja kwa watumishi ambao hawawajibiki ipasavyo. 
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kikao cha menejimenti ya ofisi yake (hawapo pichani) alipokutana nao kwa lengo kufahamiana na kupanga mkakati madhubuti wa utendaji kazi utakaoziwezesha taasisi za umma nchini kutoa huduma bora kwa umma.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha menejimenti ya Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokutana nao kwa lengo kufahamiana na kupanga mkakati madhubuti wa utendaji kazi utakaoziwezesha taasisi za umma nchini kutoa huduma bora kwa umma.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...