Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Polisi wanawake mkoa wa Arusha kupitia Mtandao wao (TPF NET) wamepongezwa kutokana na utendaji bora wa kazi zao za kila siku hasa katika suala zima la kudumisha nidhamu na kufanya kazi kwa uaminifu.

Pongezi hizo zimetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ramadhani Ng’anzi wakati wa kuhitimisha maazimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili yaliyoanza rasmi Novemba, 25 mwaka huu.  Kamanda Ng’anzi alisema kwamba, askari wa kike wamekuwa mstari wa mbele katika kuwahudumia wananchi lakini pia kudumisha nidhamu kwa kiwango cha hali ya juu katika utendaji wao wa kazi.

“Natoa pongezi kwa viongozi wenu wa TPF NET kwa kuwasimamia vyema na kuwaweka kwenye mstari mnyoofu na wale ambao walikuwa na dalili za kwenda kinyume na kazi walirudishwa kwenye njia kuu”. Alisema Kamanda Ng’anzi.

Alisema ubora wao wa utendaji kazi umekuwa kivutio kwa baadhi ya taasisi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali mkoani hapa ambapo wamekuwa wakifanya kazi pamoja nao hasa katika Madawati ya Kijinsia na Watoto kupitia harakati za kupinga ukatili na unyanyasaji na kuahidi kujenga ofisi kubwa ya Dawati mkoa itakayotoa nafasi ya faragha kwa wateja.
 Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa askari wanawake (TPF NET) mkoa wa Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi Edith Makweli akikabidhi vifaa vya usafi kwa wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya Mount Meru wakati wa maazimisho ya siku 16 za kupinga ukatili yaliyofanyika mkoani hapa.
 Baadhi ya askari wa kike mkoa wa Arusha ambao ni wanachama wa TPF NET mkoa wa Arusha wakijiandaa kugawa Khanga kwa wagonjwa waliolazwa katika moja ya wodi wa wazazi iliyopo hospitali ya rufaa ya Mount Meru wakati wa maazimisho ya siku 16 za kupinga ukatili
Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake mkoani Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi Edith Makweli akimsalimia mtoto aliyelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mount Meru pamoja na kumpa zawadi wakati wa maazimisho ya siku 16 za kupinga ukatili yaliyofanyika jana.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...