Na Mwandishi Wetu
Serikali imesisitiza uwepo wa usawa wa kijinsia katika sekta mbalimbali ili kuendelea kuunga jitihada za kuwezesha usawa huo ambao uliasisiwa katika Mkutano wa Nne wa Dunia wa Wanawake uliofanyika Beijing nchini China mwaka 1995 huku ikisisitiza ni muhimu kuundwa kwa madawati ya jinsia katika idara za serikali.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizindua Mtandao wa Wanawake na Utambulisho wa Sera ya Haki na Ulinzi wa Mtoto katika Jeshi la Magereza leo jijini Dar es Salaam .
Amesema Serikali imeweka mkazo katika kuhakikisha usawa wa kijnsia unafikiwa katika sekta na nyanja mbalimbali kwa kuchukua hatua ikiwemo kuandaliwa kwa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 pamoja na Mkakati wa Utekelezaji wake kwa lengo la kuweka mazingira muafaka na kuhakikisha kuwa masuala ya jinsia yanzingatiwa na wadau ikiwemo Wizara, Idara na Wakala za Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na Wadau wa Maendeleo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
(katikati), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (wapili kushoto), na Viongozi Waandamizi wa Jeshi la
Magereza wakikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mtandao wa
Wanawake na Utambulisho wa Sera ya Haki na Ulinzi wa Mtoto katika
Jeshi la Magereza. Uzinduzi huo umefanyika leo katika Viwanja vya
Karimjee, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu(katikati) akimkabidhi tuzo Mwakilishi wa Benki ya NMB,ikiwa ni
ishara ya kutambua mchango wa taasisi hiyo ya kifedha katika
uanzishwaji wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza
lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es
Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu(katikati), akimkabidhi tuzo mwakilishi wa Chama cha Wanasheria
Wanawake(TAWLA), ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa taasisi hiyo
katika uanzishwaji wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza
lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es
Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
akiangalia bidhaa inayotengenezwa na Jeshi la Magereza wakati
alipotembelea mabanda ya jeshi hilo wakati wa Uzinduzi wa Dawati la
Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya
Karimjee, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na Jeshi la Magereza wakati
alipotembelea mabanda ya jeshi hilo wakati wa Uzunduzi wa Dawati la
Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya
Karimjee,leo jijini Dar es Salaam..Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...