Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
KATIKA kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wamefungua kongamano la kampeni ya siku 16 za kupambana na ukatili wa kijinsia. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano hilo Mkurugenzi mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi amesema kuwa Wanawake ni nguvu kazi ya Taifa na pasipo kumthamini hakutokuwa  na Maendeleo ambayo yatakua na usawa wa kijinsia na haki sawa.

Amesema kuwa kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa mwanamke ni usalama wake na ni jukumu la kila mmoja katika kutokomeza ukatili wa kijinsia na hasa kuwalinda wanawake katika janga hilo. Kuhusiana na  rushwa ya ngono makazini hasa kwa waajiri kwenda kwa waajiriwa bi. Lilian amesema kuwa kupitia kampeni hiyo hali hiyo itavunjwa na kupigwa vita kwani elimu itatolewa kwa pande zote ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa na uhuru na ujasiri wa kusema pindi anapokutana na changamoto hizo.

Aidha amesema kuwa wao kama TNGP mtandao wataendelea kuunga mkono juhudi zote zitakazofanywa na na TAKUKURU na vyombo vingine vya dola katika kuhakikisha vita hiyo inafanikiwa na ametoa wito kwa serikali na wadau wengine kushirikiana katika kuhakikisha janga hilo la ukatili linatokomea kabisa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo ameeleza kuwa wapo bega kwa bega na serikali pamoja na vyombo vya dola katika kuhakikisha janga hilo linatokomea kabisa wakati wa kongamono hilo lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao  leo jijini Dar es Salaam.
Wadau pamoja na wadua mbalimbali kutoka vitovu vya jinsia  na Clabu za jinsia Mashuleni wakiwa kwenye kongamono la kupinga ukatili wa kijinsia lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao  leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa kamati ya wanawake (TUCTA) Rehema Ludanga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kugmfunguliwa kwa kongamano hilo ambapo amesema kuwa taasisi binafsi zinaongoza kwa rushwa ya ngono mahali pa kazi wakati wa kongamono hilo lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao  leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...