KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (Auwasa) wamezindua mfumo mpya wa malipo ya kielekroniki serikalini (GePG) katika mikoa ya Arusha , Kilimanjaro na Manyara.

Mfumo huo utarahisisha upatikanaji wa Ankara mbalimbali pamoja na kufanya malipo kutokana na huduma wanazopata kutoka taasisi za serikali zaidi ya 300 lengo ikiwa ni kurahisisha watumiaji wa huduma kutokaa katika misururu. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua mfumo huo , Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Nancy Bagaka alisema kuwa mfumo huo utapunguza kwa kiwango kikubwa ubadhirifu jambo ambalo litaongeza mapato ya serikali.

“Kutokana na mfumo huu faida nyingi zitapatikana ikiwemo kuongeza mapato ya serikali kupitia taasisi na mashirika , kuboresha uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu , utoaji taarifa za mara kwa mara pamoja na kuondoa ubadhirifu na wizi” alisema Bagaka. Aidha alisema ili kuweza kulipia Ankara mteja wa Tigo atatakiwa kupiga *150* 01# kisha atachagua kulipia ankra ambapo eneo la malipo ya serikali itajitokeza na kuingiza tarakimu 12 kwa taasisi anayotaka ipokee malipo .

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Auwasa Edes Mushi alisema kutokana na mfumo huo mpya sasa wateja wa Mamlaka hiyo hawatolazimika kukaa katika misururu mirefu wakisubiri kulipia Ankara za maji. “Auwasa kwa kushirikiana na Tigo tunaendelea kurahisisha maisha ya wateja wetu kwa kutumia mfumo huu wa GePG ambao tayari taasisi na mashirika mengi yanautumia” “Mbali na Auwasa, tayari Wizara ya Ardhi na Maenedeleo ya Makazi wanatumia, Shirika na Ndege ATCL , Bodi ya Utalii , Hospitali zote za umma , Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) Wizara ya Mifugo nk .”

“Matumizi ya mfumo huu wa kielektroniki umerahisha utoaji huduma kwa wananchi na umeleta tija kubwa na kuongeza mapato hivyo tunasisitiza wateja wa Tigo wautumie ikiwa ni pamoja na kuulizia ankara zao za malipo ya maji” alisisitiza Mushi. Mpaka sasa takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watumiaji milioni 7 wa huduma ya Tigo pesa wanafanya malipo kwa haraka bila usumbufu kwenda kwa wakala ,idara na taasisi kadha wa kadhaa za Serikali.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi akizungumza na wanahabari mjini Arusha jana kuhusu matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG) utakaokuwa ukifanywa kwa kutumia Kampuni ya Tigo kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka. 


Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka akizungumza na wanahabari hawapo pichani kuhusu uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG), mjini Arusha jana kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi. 


Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka (kushoto)akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi muda mfupi kabla ya uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG), mjini Arusha leo 
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG), mjini Arusha leo wazungumzaji wakiwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...