Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amefanya ziara mkoani Morogoro katika Wilaya za Kilombero na Malinyi ili kutatua migogoro na malalamiko ya wafugaji.

 Katika Wilaya za Kilombero na Malinyi  Ulega aliwataka wafugaji waliopo katika bonde la mto Kilombero kuondoka na kwenda kwenye maeneo waliyotengewa ili kuepusha madhara kwa mto huo ambao ndiyo chanzo muhimu cha maji ya mto Rufiji. 

Ulega alisema wafugaji hao wanapeleka mifugo hiyo bonde la mto Kilombero kufuata maji na kuagiza Halmashauri za Kilombero na Malinyi kutengeneza mabirika ya kunyweshea maji mifugo ili wafugaji wasiende kufuata maji katika bonde hilo. Aidha, aliwataka TAWA kushirikiana na Halmashauri za Kilombero na Malinyi kutengeza mabirika hayo ambapo moja ni takribani Sh. milioni 20 (birika milioni 5 na kisima Sh.milioni 15).

Pia wafugaji wa maeneo hayo walikiri kutokwenda bonde la mto Kilombero wakitengenezewa miundombinu ya mifugo hasa maji katika maeneo yao.
Ulega amesisitiza umuhimu wa kutunzwa maeneo hayo oevu ili kutunza mto Kilombero kwa lengo la kuendelee kupata maji mengi katika mto Rufiji itakayosaidia kufanikisha agenda ya Rais Dkt. John Magufuli ya mradi wa Stieglers Gorge.

Aidha,  Ulega aliwaagiza Wakala wa Mafunzo na Elimu ya Mifugo (LITA) kuandaa mafunzo ya mda mfupi kwa ajili ya wafugaji hao ili waweze kufuga kisasa wawe na mifugo wenye tija. Pia, aliwataka Serikali ya kijiji kuheshimu mipango ya matumizi bora ya ardhi iliyopo ili kuepusha migogoro.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega(wambele)akiwa ameambatana na viongozi wa wilaya Malinyi mkoa wa Morogoro wakati wakiwasili kwenye kijiji cha Ngombo,wakati wa ziara yake ya kuzisikiliza kero migogoro mbalimbali ya wafungaji,wavuvi na kuzitafutia ufumbuzi.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ngombo wilaya ya Malinyi mkoa wa Morogoro,katika mkutano wa hadhara wa  kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji,wavuvi  na kuzitatua.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wapili (kushoto) akiwa ameambatana na viongozi wa wilaya Malinyi mkoa wa Morogoro wakiwasili katika kijiji cha Ngombo kwenye ziara yake ya kuzisikiliza kero na migogoro mbalimbali ya wafungaji,wafungaji na kuzitatua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...