UMOJA wa Mataifa umesema jamii ina wakati mgumu wa kutengeneza mikakati ya kumaliza tatizo la UKIMWI ifikapo mwaka 2030 au la kizazi kijacho kitabeba mzigo mzito wa kuendelea kupambana na janga hili la kidunia. Tamko hilo limetolewa wakati inatambulika kwamba watu milioni 77 duniani wameambukizwa UKIMWI huku wengine milioni 35 wakiwa wamekufa kutokana na magonjwa nyemelezi. Kauli hiyo imetolewa juzi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani, akikariri waraka wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye siku hiyo.

Alisema miaka 30 tangu kuanzishwa kwa siku ya UKIMWI duniani, bado hali ni tete na kwamba juhudi zozote tunazochukua sasa zinaweza kuonesha kama tutazika UKIMWI ifikapo mwaka 2030 au la. Alisema pamoja na dunia kupiga hatua kubwa katika kung’amua na kutibu ugonjwa huo, hatua zilizofikiwa bado hajazifikia nia ya dunia ya kuondokana na tatizo hilo.
Katibu Mkuu huyo alisema kwamba maambukizi mapya hayapungui kwa jinsi dunia inavyotaka huku baadhi ya maeneo yakiwa nyuma zaidi huku raslimali fedha zikizidi kupungua.

Pia hali ya unyanyapaa inazidi kuwa mbaya zaidi na huduma kwa wahitaji zikiwa za kibaguzi na kusababisha kutokuwapo kwa uwazi. Katibu mkuu huyo alitaka dunia kubadilika kuondokana na unyanyapaa na ubaguzi na kuhakikisha kwamba huduma zinatolewa kuudhibiti na kuumaliza ugonjwa huo. Akizungumza katika siku ya UKIMWI mbele ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Mratibu huyo wa Umoja wa Mataifa ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI na kusema UN ipo sanjari na juhudi za Tanzania.
 Mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng  kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na UN nchini alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi jijini Dodoma. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu Mhe. Jenista Mhagama.
 Mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa akihutubia wananchi (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng akitoa salamu kutoka wa wahisani wa maendeleo wa UKIMWI wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wezee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana wa wizara hiyo wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wakiwemo wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dodoma, Maafisa wa jeshi la Polisi, wakazi wa jiji la Dodoma, Wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za serikali, viongozi wa dini pamoja wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa waliohudhuria hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.
Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wadau wa maendeleo wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kitaifa yalifanyika Desemba Mosi 2018 jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...