Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedith Kakoko, amesema mpango wa kufufua bandari bubu ambazo zipo zaidi ya 250 nchi nzima utaongeza mapato ya mamlaka kwa kiasi kikubwa sambamba na kudhibiti bidhaa za magendo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam Kakoko alisema jumla ya mapato ya bandari hizo yanakadiriwa kuweza kufikia theluthi moja au nusu ya mapato ya Bandari ya Dar es Salaam.

Bandari ya Dar es Salaam ambayo imefikia kuhudumia shehena za tani milioni 16.2 kwa mwaka inaingiza Sh bilioni 70 kwa mwaka kwa mujibu wa takwimu za TPA za mwaka 2017.

Kakoko alisema zipo hatua kadhaa zinazochukuliwa katika mpango wa kufufua bandari bubu ikiwemo kuzianisha, kuwashirikisha wadau, kuzifanyia tathmini, kuandika ripoti ya kuanisha bandari zenye sifa za kuweza kufufuliwa na kisha kuipeleka kwa wizara husika kwaajili ya mapitio na kupitishwa.Alisema kwa sasa zoezi la kuzitambua na kuzianisha zinaendelea na kwamba zoezi hilo linatarajia kukamika mwezi huu, "tunatarajia zoezi likikamilika tunaweza kupata bandari bubu zaidi ya 300."

"Tayari tumeshafanya vikao na wakuu wote wa mikoa na wilaya ambazo zina bandari bubu na nusu ya viongozi wote wa vijiji na kata katika maeneo hayo tayari tumeshazungumza nao na zoezi hilo linaendelea," alisema Kakoko.

Alisema ushirikishwaji huo wa wadau umefanyika ili kupata ushirikiano katika utekelezaji wa usimamizi wa bandari hizo pindi zitakaporasimishwa na kutopata mapingamizi.Kuhusu gharama za kuendesha bandari hizo pindi zitakaporasimishwa alisema kwa kiasi kikubwa hazihitaji gharama kubwa kwani zitakodishwa kwa halmashauri, vijiji au watu binafsi ili kuziendesha na kukusanya mapato kwa niaba ya TPA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedith Kakoko, akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya urasimishaji wa bandari Bubu na Umuhimu wake katika kukuza pato la Taifa.
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedith Kakoko .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...