Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
MGANGA Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi amesema viwanda vya dawa vinahitaji watalaam wenye msingi wa Masomo ya Kemia na Biolojia. Profesa Kambi ameyasema hayo leo wakati wa utoaji tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya Biolojia na Kemia katika matokeo ya kidato cha Nne na Sita kwa mwaka 2018 iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa nchi inaelekea katika uchumi wa viwanda ambapo vitajengwa viwanda vya dawa hivyo kunahitajika wabobezi wa katika masomo ya Kemia na Biolojia kwa ajili ya kuendesha viwanda hivyo. Aidha amesema kuwa masomo hayo wanatakiwa wanafunzi kujituma zaidi ikiwa na wazazi kuwatia moyo wa kufanya vizuri katika masomo ya sayansi. Profesa Kambi amempongeza mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuanzisha tunzo hizo kwani inawatia moyo wanafunzi kuendelea kuvutika katika kusoma masomo ya Kemia na Biolojia.

Nae Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa wamekuwa wakitoa tunzo kwa wanafuzi kwa kuwapa cheti pamoja na Fedha. Amesema kwa huu jumla ya wanafunzi waliopata cheti na fedha ni 24 na walimu wanne wa masomo hayo. Wanafunzi hao wamepata kuanzia sh.500000 hadi 350 kwa wakwanza hadi wa tatu.  Amesema katika matokeo hayo shule za serikali ni Nne ambazo zimetoa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia na Biolojia kwa mwaka 2018.

 Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi akizungumza wakati wa utoaji tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya kidato cha Nne na Sita mwaka 2018 iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mkemia Mkuu wa serikali wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza kuhusiana utoaji tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha Nne na Sita mwaka 2018 katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Esther hellen Jason akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tunzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya kidato cha Nne na Sita iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi akimkabidhi Cheti  Mwanafunzi aliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha Nne katika Masoko  Biolojia na Kemia Liliani Katabalo katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam.
 Mgeni Rasmi Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Kambi akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani ya Biolojia na Kemia kwa kidato cha Nne.
KUSOMA ZAIDO BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...