Vodacom, kampuni nambari moja ya mawasiliano ya simu nchini imeungana na kampuni ya Tecno kuwaletea wateja wao toleo jipya la simu aina ya Tecno Camon 11, leo jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huu ni harakati ya Vodacom kuhakikisha jitihada zake za kuwezesha maisha ya kidijitali kwa wateja wao, kwa kupitia simu janja zinafanikiwa. 

Akizungumza na waandishi wakati wa uzinduzi wa simu hiyo, Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Bw. Eric Mkomoya alisema, “Tumedhamiria kuhakikisha kila Mtanzania anamiliki simu janja na kwa pamoja tunalifanya taifa la Tanzania kuwa la kidigitali”. Uzinduzi huu uliohudhuriwa na wateja lukuki utawawezesha watumiaji wa matoleo ya awali wa simu za TECNO Camon kuweza kubadili simu zao ili kujipatia toleo hili jipya kwa kuongeza kiasi kidogo cha pesa. 

Simu hii inapatikana kwa bei ya shilingi laki nne tu (Sh. 400,000) na inakuja na Intaneti ya GB 15 ambapo mteja anapata GB tano kwa miezi mitatu mfululizo. TECNO Camon 11 ina kamera ya mbele yenye uwezo wa mega pixel 16 na kamera mbili za nyuma yenye uwezo wa mega pixel 13 na 2 kwa picha bora zaidi. Simu hii pia ina uwezo wa 4G LTE pamoja na uwezo wa kuhifadhi laini mbili za simu.

Pamoja na hayo, simu hii ina flashi iliyotengenezwa kwa rangi maalumu kuweza kusaidia mwanga kutoka vizuri huku ikiwa na kioo chenye ukubwa wa inchi 6.2 chenye uwezo wa FHD. Maduka yote ya TECNO yatatoa si huduma za TECNO tu bali pia kusajili laini za Vodacom. 
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (wa pili kushoto) akimkabidhi zawadi ya simu mpya ya Tecno Camon 11Pro, kwa mhamasishaji wa Tecno Abdallah Sultan 'Dullivan' wakati wa uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Simu hiyo itauzwa katika maduka ya Vodacom kwa kiasi cha TSh. 400,000. Kushoto ni Meneja wa Maduka ya rejareja ya Vodacom, Happiness Macha na  Meneja Uhusiano wa Tecno Erick Mkomoya kulia.
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (katikati) akiwaonesha waandishi wa habari ( hawapo pichani) simu mpya ya Tecno Camon 11pro wakati wa uzinduzi wa simu hizo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Simu hiyo itauzwa katika maduka ya Vodacom kwa kiasi cha TSh. 400,000. Kushoto ni Meneja wa Maduka ya rejareja ya Vodacom, Happiness Macha na Meneja Uhusiano wa Tecno Erick Mkomoya.
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (wa pili kushoto) akimkabidhi mpiga picha wa ITV Goodluck Maruti (kulia) zawadi ya simu mpya ya Tecno Camon 11pro, mara baada ya kuibuka mshindi wakati wa uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Simu hizo zitakazouzwa katika maduka ya Vodacom kwa kiasi cha TSh. 400,000 tu. Kushoto ni Meneja wa Maduka ya rejareja ya Vodacom, Happiness Macha na Meneja Uhusiano wa Tecno Erick Mkomoya.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...