Na Benny Mwaipaja,WFM, Simiyu

ZAIDI ya Wakazi elfu 2 wa Mji wa Lagangabilili, Tarafa ya Kanadi, Wilayani Itilima, mkoani Simiyu, wameondokana na adha ya kukosa maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi wa maji ya bomba wa Lagangabilili uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 900.

Wakizunguza mbele ya timu maalumu ya wataalam wanaofuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka baadhi ya Wizara wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Baadhi ya wakazi wa Mji huo wa Lagangabilili wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mradi huo wa maji.

“Tunaishukuru sana Serikali kwa kutuletea maji tunayapata kwa urahisi, zamani tulikuwa tukihangaika sana akina mama walikuwa wakiyafuata mto Simiyu, mbali sana, walikuwa wakitoka saa kumi usiku na kurudi saa tatu asubuhi” alisema Bw. Chonza Maduhu, mkazi wa Lagangabilili, Simiyu
Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Itilima, Bw. Goodluck Masige, amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kumefanya kiwango cha upatikanaji maji safi na salama kwenye mji huo ambao ndio makao makuu ya wilaya ya Itilima, kupanda kutoka asilimia 20 za awali hadi kufikia asilimia 100.

“Tumejenga tenki lenye ujazo wa lita 225,000, vituo 21 vya kuchotea maji, tumejenga mtandao wa bomba za kusambaza maji nyenye urefu wa mita 29,000 na kufunga pampu 1 ya kusukuma maji” aliongea Mhandisi Masige
  

Mhandisi Christer Mchomba (mwenye kofia), kutoka Wizara ya Maji, akiandika maelezo ya Mhasibu wa Kamati ya Maji ya Mji wa Lagangabilili, Bi. Kundi Paulo, wakati Timu Maalum ya Serikali ikiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, ilipokuwa katika Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 
3-min
Mkazi wa Mji wa Lagangabilili, Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Bi. Pendo Tindigwe, akiwa amebeba ndoo yake yenye maji baada ya kukamilika kwa mradi wa maji Lagangabilili uliojengwa na Serikali kwa gharama ya Sh. 907m.
4-min
Tenki la maji la Mradi wa Maji wa Mji wa Lagangabilili, Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, lenye uwezo wa kubeba lita 225,000 za maji kwa wakati mmoja kwa ajili ya kuwahudumia wakazi 2,212 wa Mji huo wa Lagangabilili.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...