Na John Nditi, Morogoro
NAIBU waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye ameiagiza Baraza la Wafanyakazi  la Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) pamoja na   Menejimenti ya  Kampuni  kuimarisha kitengo cha masoko na kufanya ufuatiliaji  kwa watumishi  na mawakala wanaoihujumu Kampuni  hiyo.
Naibu Waziri alisema hayo  katika hotuba yake ya   ufunguzi wa kikao cha tatu cha  baraza la wafanyakazi wa ATCL lililofanyika  mjini Morogoro.
 Alisema , kwa muda mrefu kumekuwa na  manenoo mengi yanayosemwa juu ya kuwepo hujuma dhidi ya  Ndege za ATCL   hasa kwenye  njia  ya Kilimanjaro na Mbeya .Mbali na njia hizo pia huduma hizo zinafanywa kwa maeneo mengine ambapo wateja wanapohitaji huduma za  ATCL huambiwa kuwa ndege zimejaa wakati  jambo hilo si kweli na matokeo yake ndege zinaondoka bila kujaa abiria.
“ Baadhi ya makawala wanaouza tiketi za ATCL wanaonwa na makampuni mengine ya Ndege  ili wajaze kwanza ndege  zao kwa kutoa maelezo kwa wateja wanaohitaji kusafiri na ndege zetu za umma kuwa zimejaa , lakini baadaye zinaondoka bila kujaa abiria” alisema Naibu Waziri Nditiye.
Naibu Waziri huyo alisema “ Huduma za ndege zetu ni nzuri  na nauli yake ni ndogo  na pia ndege zetu zote ni mpya lakini hazijai  tofauti na za makampuni binafsi ambayo bei zake ni za juu na huduma zao hazifanani na za ATCL “ alisema Naibu Waziri Nditiye .
 Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye ( kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi mkuu wa ATCL,  Ladislaus Matindi  ( wa pili kushoto ) baada ya Naibu Waziri kufungua   kikao cha tatu cha  baraza la wafanyakazi wa ATCL lililofanyika  mjini Morogoro.
 Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Atashasta Nditiye ( kulia ) akijadiliana jambo  na  Mkurugenzi mkuu wa ATCL,  Ladislaus Matindi  (  kushoto ) kwa ajili ya kufungua  kikao cha tatu cha  baraza la wafanyakazi wa ATCL kilichofanyika  mjini Morogoro.
 Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa ATCL wakimsilikiza  Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye (  hayupo pichani ) alipofungua  kikao cha tatu cha  baraza  hilo  mjini Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...