Ikiwa zimesalia siku chache kabla ya kumalizika kwa robo ya kwanza, ya Kampeni ya Toharakinga kwa Wanaume wenye umri kuanzia miaka kumi na kuendelea inayoendeshwa mkoani Geita, kundi la wanawake limebainika kuwa chachu ya kufanikisha mpango huo kutokana na wengi wao kuwahimiza wanaume wao na watoto kwenda kufanyiwa Tohara.

Hadi kufikia Sepetemba 2018, wanaume 115, 000 kati ya 119, 000 waliolengwa kufanyiwa tohara Mkoani Geita walikuwa wamefikiwa na kuhudumiwa katika kampeni inayoendeshwa na Serikali kwa ushirikiano na Shirika lisilo la kiserikali la IntraHealth International kwa ufadhili wa Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) PEPFAR kupitia CDC,

Kituo cha Afya Katoro ni kati ya vituo 23 vya muda na 13 vya kudumu vinavyotoa huduma hiyo ambayo kabla ya kutolewa wanaume wanaofika kufanyiwa tohara hupitia hatua kadhaa ikiwemo kuandikishwa, kuelimishwa na kupimwa virusi vya UKIMWI kabla ya huduma.

Msimamizi wa Kituo hicho, Bw. Faustine Edward alisema muitikio wa wananchi umekuwa mkubwa kiasi cha kuwafanyia tohara wanaume kati ya 10 hadi 30 kwa siku.

“Mwitikio ni mkubwa sana, wateja ni wengi, hadi tunafikiria kuongezewa muda kwakuwa tulianza zoezi hili mwezi Novemba 15, 2018 na mwisho ni mwezi Desemba 15, 2018; Lakini pia niwapongeze akinamama, wamekuwa mabalozi wazuri kwa kuwaleta watoto wao lakini pia kuwashawishi waume zao kuja kufanya Toharakinga salama hadi kutuwezesha kupata watu 10 hadi 30 kwa siku,” alisema Bw. Edward
Wakazi wa Katoro wakisubiri kupata huduma ya Tohara ya bila malipo, inayotolewa na Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na masuala ya Afya ya IntraHealth katika kituo cha afya Katoro.

Madaktari wakimtahiri mmoja wa wakazi wa Katoro,wakati wa huduma hiyo ya bila malipo inayotolewa na Taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya Afya ya IntraHealth katika kituo cha afya Katoro.

Msimamizi wa kituo cha Tohara cha Katoro Bw. Faustine Edward, akizungumza na wakazi wa Katoro waliojitokeza kupata huduma hiyo ya bila malipo, inayotolewa na Taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya Afya ya IntraHealth katika kituo cha afya Katoro, ambapo wanatahiri watu 20 hadi 30 kwa siku. Hapa hupewa elimu kabla ya kufanyiwa tohara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...