Watumishi wa serikali kutoka idara mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi -CCM, wameandamana kumpongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya ya kizalendo na kutetea wakulima kwa kupambana na wanyonyaji ambao wamekuwa wakitajirikia jasho lao na wao kubaki maskini.

Maandamano hayo yamefanyika leo Jumapili Desemba 2,2018 kutoka katika Soko Kuu la mjini Shinyanga hadi kwenye ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kufikisha ujumbe wao kwa Rais Magufuli za kuunga juhudi za utendaji wake kazi. 

Akizungumza mara baada ya kumaliza maandamano hayo. Msemaji wa umoja huo wa watumishi wa Serikali ambao ni makada wa CCM Christopher Malengo,sambamba na kutoa tamko lao mbele ya katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa, amesema wameguswa na kazi ya kizalendo ambayo anaifanya Rais Magufuli ya kupigania maslahi ya wanyonge wakiwamo wakulima.

 Amesema Rais Magufuli amekuwa akijikita katika misingi ya ujamaa,utu,uzalendo na haki kama alivyokuwa akifanya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye utawala wake, katika kuhakikisha anapigania maslahi ya wanyonge na kukomesha wanyonyaji ili wananchi wote waweze kupata haki sawa, vitendo ambavyo zinapaswa kupongezwa.
Watumshi wa Serikali katika idara mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambao ni Makada wa Chama Cha Mapinduzi CCM wakiwa kwenye maandamano ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake mzuri wa kizalendo hasa kupigania maslahi ya wakulima,huku wakiwa wamebeba mabango ya pongezi hizo. Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachwambwa akipokea mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kumpongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake kazi hasa kupigania wanyonge ili kuwainua kiuchumi. Upokeaji wa mabango ukiendelea. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...