Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amesema China ndio nchi pekee ambayo imeweka fedha nyingi zaidi kwa ajili ya uwekezaji ambapo fedha waliyoweka kwenye kuwekeza ni Dola za Marekani bilioni 5.8 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh.trilioni 12 huku akisisitiza umuhimu wa kujengwa kwa viwanda nchini ambako kutsaidia kuzalisha bidhaa nyingi ambazo zitauzwa nje ya nchi yetu.

Kakunda amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati mkutano uliowakutanisha wawekezaji kutoka nchini China, maofisa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na wadau mbalimbali wa sekta zinazojihusisha na uwekezaji nchini ambapo wametumia nafasi hiyo kujadili fursa za uwekezaji ambazo zipo nchini.

Akifafanua zaidi wakati anazungumzia ujio wa wawekezaji kutoka nchini China ambao wapo nchini kuangalia fursa za uwekezaji, amesema kuwa kwa sasa China ndio nchi ambayo imeweke fedha zake nyingi kwa ajili ya masuala ya uwekezaji ambao wamewekeza nchini.

"Nchi ya China au wawekezaji kutoka China ndio ambao wameka fedha nyingi sana katika maeneo ya uwekezaji.Wamewekeza kwenye viwanda vya aina mbalimbali, vimo viwanda vya saruji, viwanda vya kubangua kurosho na pia wapo pia kwenye uwekezaji katika eneo la ujenzi ambako nako huko wameweka fedha nyingi,"amesema Kakunda.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini Tanzania(TIC)Geoffrey Mwambe (kulia) akiteta jambo na Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Wang Ke wakati wa kongamano la uwekezaji ambalo limejumuisha wawekezaji wa nchi hizo mbili
 Mwenyekiti wa Baraza la Kukuza Uhusiano kati ya nchi zinazoendelea kutokana China Lyu Xinhua akizungumza kwenye kongamano la uwekezaji kati ya wawekezaji wa China na Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda (kushoto)akiandika kabla ya kuzungumza kwenye kongamano la uwekezaji ambalo liliwahusisha wawekezaji kutokana nchini China ambao wamefika nchini kuangalia fursa za uwekezaji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi(TPSF) Godfrey Sembeye akizungumza kwenye kongamano la uwekezaji baina ya wawekezaji waChina na Tanzania ambalo limefanyika leo jiiini Dar es Salaam.
 Baadhi ya  wawekezaji kutoka nchini China ambao wapo nchini wakiangalia fursa za uwekezaji wakimsikiliza Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseoh Kakunda wakati wa kongamano la uwekezaji kati ya China na Tanzania.wakimsiki.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...