Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amezindua mradi wa vioski tembezi wa kampuni ya Sigara Tanzania (TCC).

Akizungumza leo Disemba 8, 2018 Waziri Mhagama amesema kuwa mradi huo utasaidia wajasiriamali wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo kuweza kujiajiri na kupata kipato kitakacho wanufaisha kiuchumi.“Hii ni faraja kubwa kwetu kama Serikali kuona mnaunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto za ajira nchini kwa kuwawezesha wajasiriamali kuchangamkia fursa za kujiendeleza kibiashara”, alisema Mhagama.

Aliongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa wadau na kuwataka wawekezaji wengine waweze kubuni miradi kama hiyo yenye manufaa kwa wananchi.Aidha, Mhe. Mhagama aliipongeza kampuni ya Sigara Tanzania kwa ubunifu na kuwasihi waendelee kufanya vizuri katika nyanja nyingine kwa manufaa ya watanzania kwa ujumla.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa ni jambo la faraja mradi huo umezinduliwa Jijini Dodoma ikiwa ni fursa kubwa kwa wajasiriamali kuweza kunufaika kiuchumi.

Naye, Mkurugenzi wa Masoko, Bi. Awaichi Mawalla amesema kuwa Vioski 400 vitagawiwa nchi nzima kwa wajasiriamali wadogo ambao wamekuwa wakifanya kazi na kampuni ya TCC na wataweza kuuza bidhaa mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo wa vioski wa kampuni ya Sigara Tanzania (TCC). (Kushoto) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa pamoja na Naibu Waziri Mhe. Anthony Mavunde (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) wakimsikiliza Fundi Mkuu wa Vifaa Saidizi kwa Watu wenye Ulemavu Bw. Mwita Marwa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa Viungo Dodoma, Bw. Hassan Hussein.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali walioweza kunufaika na mradi huo, mara baada ya uzinduzi wa hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma, Disemba 8, 2018.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...