WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekitaka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimalize urasimu ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. Kadhalika, ameuagiza uongozi wa TIC uweke kipaumbele cha kwanza katika kulinda rasilimali za nchi na maliasili zake ikiwemo ardhi, mazao ya uvuvi, misitu, madini.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo jioni (Jumanne, Desemba 4, 2018) alipozungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa TIC na Menejimenti, jijini Dar es Salaam. “Katika kuvutia wawekezaji hasa wa nje ni lazima tuweke kipaumbe katika kulinda rasilimali zetu kama ardhi, madini fukwe ili zisiporwe kwa kisingizio cha uwekezaji.” 

Amesema eneo hilo linahitaji umakini na uadilifu mkubwa, hivyo ni muhimu kwa kituo hicho kuhakikisha kinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia maslahi ya Taifa. Amesema ili kupata matokeo mazuri ni lazima waimarishe mawasiliano na uratibu miongoni mwa wadau wote sambamba na kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa.

“Serikali imedhamiria kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025, TIC inatakiwa iongoze kwa kuvutia wawekezaji wengi wa ndani na nje ya nchi.” Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa wawekezaji ambao TIC inatakiwa ivutie ni walio mahiri wenye nia thabiti ya kutufikisha huko na siyo wachuuzi au madalali. 

Kadhalika,Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inataka TIC iwe kioo cha nchi ambacho kitavutia wawekezaji. Amesema Serikali inataka TIC mpya ambayo itakuwa kimbilio la wawekezaji wengi wa ndani na nje, badala ya kuwa kikwazo na kusababisha wawekezaji wakija kukimbilia.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Watendaji, kwenye Ofisi za Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwenye viwanja vya Ofisi za Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa, Faustine Kamuzora na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, Afisa wa NEMC katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Linda Mutafungwa wakati alipotembelea Kituo hicho, Desemba 4, 2018. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa wa Kodi na Forodha wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Leonard Mapunda (wapili kulia) na Helen Haule (kulia) wakati alipotembelea Kituo hicho, Desemba 4, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa wa Kodi na Forodha wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Leonard Mapunda (kulia) na Helen Haule ( wapili kulia) wakati alipotembelea Kituo hicho, Desemba 4, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Wajumbe wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakati alipotembelea Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...