WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu wananchi hususan wakulima wa korosho nchini baada ya kuwahakikishia kuwa korosho zao zote zitanunuliwa. Amesema Serikali kupitia Bodi ya Mazo Mchanganyiko itanunua korosho zote na hakuna korosho za wakulima nchini ambazo zitabaki bila ya kununuliwa.
Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Desemba 7, 2018) alipozungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha korosho cha Terra akiwa njiani kwenda Dodoma. Waziri Mkuu amesema bodi hiyo inaendelea kufanya thamini na kujiridhisha kama kweli korosho hizo zimezalishwa nchini na kuangalia viwango vya ubora.
Amesema baada ya kujiridhisha kuhusu viwango vya ubora na mkulima aliyepeleka ndiye mwenyewe ndipo taratibu za malipo hufanyika. Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kununua korosho baada ya wafanyabiashara kutaka kuzinunua kwa bei ya chini ambayo haikuwa na tija.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipotembelea kiwanda cha
korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evaresti Ndikilo akizungumza kabla ya
kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili azungumze wakati Waziri
Mkuu alipotembelea kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa
Mathias, Desemba 7, 2018.
Wafanyakazi
wa kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya
kutembelea kiwanda hicho, Desemba 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Meneja Uzalishaji wa
Kiwanda cha Korosho cha Terra Cashew, Leonardo Denti (wapili kulia)
wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kibaha kwa Mathias, Desemba
7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...