*Awataka waliopewa dhamana wazingatie viwango vya kimataifa
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezinduaChaneli ya Taifa ya Utalii iitwayo Tanzania Safari Channel na amewataka watu wote waliopewa dhamana ya kuiendesha wahakikishe wanazingatia viwango vya kimataifa katika vipindi watakavyokuwa wanaviandaa. “Vipindi vyenu ni lazima vivutie kama vile tunavyoviangalia katika chaneli za wanyama za kimataifa kama vile National Geographic, Discovery, Travel na zingine ili lengo lililokusudiwa wakati wa kuanzishwa kwake litime.”
Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Desemba 15) wakati akizindua chaneli hiyo kwenye Ofisi za TBC, Mikocheni, jijini Dar es Salaam, ambapo ametoa wito kwa Wizara zote zinazohusika na uanzishwaji wa Chaneli hiyo kuhakikisha zinailea wakati ikijijenga kujiendesha kibiashara.
Amesema Tanzania ni moja ya nchi duniani zilizotenga moja ya tatu ya eneo lote la nchi kwa ajili ya uhifadhi, ambapo kuna tamaduni za makabila mbalimbali, ngoma za kuvutia, vyakula vya asili, sinema za maisha yetu na lugha adhimu ya Kiswahili.
“Hivyo, kwa kuanzishwa kwa chaneli hii inayotengeneza vipindi na kuonesha vivutio hivi ndani na nje ya Tanzania itasaidia watalii huko waliko kujua huu utajiri wetu na kuchagua kuja kutalii nchini. Ni matumaini yangu kuwa hii Tanzania Safari Channel ninayoizindua leo itaongeza thamani katika kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea Tanzania.”
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Chaneli ya Tanzania Safari Channel
kwenye Viwanja vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es
salaam Desemba 15, 2018. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC,
Dkt. Ayoub Ryoba.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Chaneli ya Tanzania Safari Channel
kwenye Viwanja vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es
salaam Desemba 15, 2018. Kushoto ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni
na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, wapili kulia ni Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC,
Dkt. Ayoub Ryoba.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ufundi
wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Upendo Mbele wakati
alipotembelea Studio mpya za TBC kabla ya kuzindua chaneli ya Tanzania
Safari Channel, Desemba 15, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt.
Ayoub Ryoba.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Chaneli ya
Tanzania Safari Channel kwenye viwanja vya Ofisi za Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC), Mikocheni jijini Der es slaaam, Desemba 15,
2018.
Baadhi
ya viongozi na wageni waalikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa wakati alipozindua Chaneli ya Tanzania Safari Channel kwenye
viwanja vya Ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es
salaam, Desemba 15, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya kuzindua Chaneli ya
Tanzania Safari Chanmnel Kwenye viwanja vya TBC, Mikocheni jijini Dar
es salam, Desemba 15, 2018. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...